• Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Complains |
Karatu District Council
Karatu District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dhamira na Dira
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Ujenzi
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
    • Vitengo
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
  • Madiwani
  • Miradi
    • TASAF
    • BOOST
  • Machapisho
    • Hali ya Uwekezaji
      • Business License Form
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Habari
    • Hotuba kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha

BODI YA AFYA WILAYA YATOA MAAZIMIO MATANO YA KIMKAKATI

Posted on: April 1st, 2020

Na Tegemeo Kastus

Mwenyekiti wa bodi ya afya ameitaka timu ya usimamizi ya afya wilaya ya Karatu kumsaidia Mganga Mkuu wa wilaya kwa kumpa taarifa za vituo vyote vya afya. Hiyo itasaidia kuongeza  uwajibikaji katika idara ya afya na kusaidia kutatua changamoto kwa wakati.

Mwenyekiti ndugu Joseph Fisso amesema hayo wakati bodi ya afya na wajumbe wake walipokaa kikao katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Karatu. Ndugu Fisso ameomba wajumbe kuendelea kushikamana na kuimarisha huduma za afya. Amesema mgawanyiko wa wafanyakazi wa afya kipindi cha nyuma ulisababisha huduma za afya kutoridhisha, kwa sasa mgawanyiko hakuna na huduma zinaendelea kuimarika siku hadi siku. Madaktari wamezidi kutoa huduma nzuri kwa wananchi na ameombwa watendaji wa chini wa afya kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma.

Ndugu Fisso ameomba Mganga Mkuu kuwa mkali kwa watendaji wa chini yake. Amesema utatuzi wa changamoto za afya siyo rahisi kama watu wa nje wanavyofikiri, kuna ugumu wake lakini tunaweza kutumia timu ya usimamizi wa huduma za afya kufanya ukaguzi wa afya kwa kila kituo cha afya. Amesema timu ya usimamizi wa huduma za afya ikifanya kazi vizuri,  na ikatoa taarifa za kutopatikana kwa dawa kwa wakati zitamfikia Mganga Mkuu mapema na kufanyia kazi.

Naye Dkt Mustafa Waziri Mganga Mkuu wa wilaya amesema kuna mambo yamefanyika mazuri, amesema kuna wafanyakazi wa idara ya afya 89 wamepandishwa madaraja. Amesema ukusanyaji wa damu wilaya ya Karatu umeongezeka sana na imekuwa ni Halmashauri inayoongoza katika ukusanyaji wa damu kuliko wilaya nyingine za mkoa wa Arusha.

Wajumbe wa bodi ya afya wakiwa katika kikao ukumbi wa Halmashauri

Dkt. Mustafa waziri amesema azimio la kwanza katika kikao hicho cha bodi ya afya ya wilaya ni kuitisha kikao cha wadau wa afya juu ya upatikanaji wa dawa za kunyunyizia katika maeneo mbalimbali Karatu ili kuchukua tahadhari ya virusi vya ugonjwa wa corona. Amesema azimio la pili kuhakikisha kila kituo cha afya au zahanati eneo la mipaka yake inapimwa ili kuondoa migogoro ya ardhi. Azmio la tatu ni kupanga dawa na kubandika orodha ya dawa zinazopatikana kwa kila kituo cha afya na zahanati. Azimio la nne ni kufanya ukaguzi wa dawa kwa kila  kituo na zahanati. Azimio la mwisho ni kuandaa madeni ya MSD kwa kila kituo kinachodaiwa na kuwapa mda wa kulipa.

Dkt, Heriel Zacharia Mganga Mfawidhi Hospitali teule ya wilaya (CDH) amesema fedha million 59 wanazopata kutoka serikalini (basket Fund) kwa kila robo wanatumia mgawanyo million 40 kwa ajili ya dawa na kiasi kinachobakia kinatumika kwa ajili ya mafuta ya ambulance na malipo ya watu wanaopeleka vifaa. Dkt. Zakaria amesema hospitali teule ya wilaya ina wastani wa kupokea watu wa bima ya afya takriban 700 mpaka 800 kwa mwezi. Dkt. Zakaria amesema fedha za serikali zinatumika vizuri ila changamoto ipo kwa watu wa bima ya afya na fedha nyingine zinazoingia kama ruzuku zianachelewa kulipwa  kwa wakati.

wajumbe wa bodi ya afya wilaya katika matukio mbalimbali kwenye Kikao.

Matangazo

  • Matokeo ya upimaji wa Kitaifa kidoto cha pili January 07, 2024
  • Halmashauri ya Wilaya ya Karatu Uchaguzi wa Wanafunzi wa kidato cha kwanza, 2024 December 18, 2023
  • Matokeo ya Darasa la Nne January 07, 2024
  • KIKAO CHA BARAZA LA MADIWANI 2024 May 11, 2024
  • Angalia Zote

Taarifa Mpya

  • MAAFISA UANDIKISHAJI WALA KIAPO KARATU

    May 14, 2025
  • DED HOKORORO ASHIRIKI KIKAO CHA ALAT WILAYA YA MERU

    May 15, 2025
  • MADAKTARI BINGWA WA SAMIA AWAMU YA TATU WATUA KARAU

    May 12, 2025
  • KARATU WASAPOTIJUHUDI ZA RAIS SAMIA WATANGAZA UTALII WA NDANI

    May 11, 2025
  • Angalia Zote

Video

DC KOLIMBA ATATUA KERO TARAFA YA EYASI KARATU
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fursa za Uwekezaji

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Wizara ya Fedha na Mipango
  • Jamvi la Habari
  • Tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karatu District Council

    Sanduku la Posta: P.O Box 190

    Simu: +255 272970648

    Simu ya Mkononi: 0754773947

    Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa