• Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Complains |
Karatu District Council
Karatu District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dhamira na Dira
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Ujenzi
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
    • Vitengo
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
  • Madiwani
  • Miradi
    • TASAF
    • BOOST
  • Machapisho
    • Hali ya Uwekezaji
      • Business License Form
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Habari
    • Hotuba kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha

HATUTAKI DIVISON ZERO KARATU

Posted on: March 9th, 2021

Na Tegemeo Kastus

Wilaya ya karatu hatutaki ufaulu wa daraja sifuri katika mtihani ya kitaifa wa kidato cha nne na mitihani wa kidato cha pili. Ufaulu wa mwanafunzi unaanza kwa mwanafunzi kupata ufaulu wa  alama D mbili ni jambo linalowezekana kufanyika.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa wilaya ya Karatu Mh. Abbas Kayanda alipokuwa akikabidhi viti  75 na meza 75 vilivyotengenezwa na wazazi katika kukabiliana na changamoto za upungufu wa madawati. Meza na madawati pamoja na ukarabati wa madarasa mawili yamegaharimu million  5250000, amesema wazazi wa vijiji vya kilimamoja, huduma na chemchem wamefanya hivyo ili kuunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mh. Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika utoaji wa elimu bure kuanzia  shule ya msingi na mpaka kidato cha nne kwa  sekondari.

Mh.  Abbas Kayanda akwa katika picha ya pamoja na wanafunzi, walimu na uongozi wa serikali ya vijiji vitatu baada ya kukabidhi madawati kwa uongozi wa sekondari Kilimamoja.

Mh. Kayanda amesema faraja pekee wanayopata wazazi ni kuona vijana wao wanafaulu, na wanaendelea na elimu ya juu. Amesema wanafunzi wametengenezewa mazingira mazuri zaidi ya kusoma lazima sasa walimu waongeze jitihada katika kuondoa daraja sifuri. Ameongeza kusema kama ufaulu utaongezeka hata shida ya ujenzi wa jengo la utawala inaweza kutatulika. Wazazi watapata moyo wa kuendelea kujitoa kwa ajili ya watoto wao, ameomba walimu kuongeza ufuatiliaji wa wanafunzi kwa  kushirikiana na wazazi pindi wanapobaini changamoto za mtoto katika maendeleo yake ya kitaaluma.

Mh. Kayanda amepongeza uongozi wa serikali ya kijiji kwa  kusimamia maagizo ya serikali ya kukarabati na kumalizia ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa. Amesema ukarabati wa ujenzi wa vyumba vya madarasa umezingatia vigezo na umetoa picha nzuri kwa  serikali na umesaidia kuondoa changamoto ya uhaba wa vyumba vya madarasa.

Mh. Kayanda ametumia fursa hiyo kuwaasa wanafunzi kusoma kwa bidii na kuzingatia masomo ili kupata matokea mazuri.a Amesema taifa linauhitaji wa wataalamu mbalimbali na wataalamu wanajengwa kutoka shuleni, ametoa rai kwa wanafunzi kuweka mkazo mkubwa katika masomo.

Mh. Abbas Kayanda akizungumza na wanafunzi wa shule ya  msingi Africa Galleria baada ya kuwakabidhi madawati

Katika ziara hiyo Mkuu wa wilaya ya Karatu Mh. Abbas Kayanda ametembelea shule msingi ya Africa Galleria na kukabdidhi madawati 65 yaliyojengwa muwekezaji wa Africa Gallleria. Madawati hayo yamesaidia kupunguza changamoto ya uhaba wa madawati katika shule hiyo ya msingi. Amempongeza muwekezaji Africa Galleria kwa kukumbuka kurudisha kwa jamii, jambo ambalo linazidi kujenga mahusiano chanya na jamii.

Akiwa katika shule ya Msingi Kainam Rhotia Mh. Kayanda amekabidhi madawati 48 ambayo yamejengwa na kukarabatiwa na wazazi katika shule hiyo. Mh. Kayanda amepongeza  wazazi kwa kuwa na mutikio chanya na kuhamasishana katika shughuli za maendeleo lengo likiwa ni kusaidia taasisi zinazozunguka maeneo yao.

Mh. Abbas Kayanda akizungumza na wanafunzi wa Kainam Rhotia baada ya kuwakabidhi madawati

Sambamba na kutembelea miradi ya elimu Mh. Abbas Kayanda ametembelea zahanati ya Kainam Rhotia ambayo imepewa kiasi cha million sita kwenye fedha za mfuko wa jimbo kwa ajili ya ujenzi wa kichomea taka, ukarabati wa maabara na ujenzi wa jengo la choo. Mh. Kayanda ameelekeza uongozi wa Halmashauri ya kijiji kuepuka matumizi mabaya ya ununuaji wa vifaa vya ujenzi. Amesema kumekuwa tabia ya watendaji kuweka gharama kubwa za Quotation za miradi, gharama ambazo haziendani na bei ya uhalisia ya ujenzi wa jengo. Ameelekeza wataalamu kujiridhisha thamani ya bei za ununuaji wa vifaa vya ujenzi. Ameeleza uongozi wa kijiji kusimamia na  kuhakikisha huduma ya nishati ya umeme inaunganishwa katika zahanati hiyo mapema.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo diwani wa kata ya Rhotia Mh.Marsel Magasi amesema ziara ya mkuu wa wilaya imezidi kuwapa hamasa ya kusimamia shughuli za maendeleo. Amesema ili kata iwe na uwezo wa kufanya shughuli zake lazima kuwe na ushirikiano wa viongozi wakijiji katika kila eneo ambao watasaidia  kuibua na kutatua changamoto zitakazowasilishwa katika ngazi ya kata.

Mh. Magasi ameshukuru wananchi wa kata ya Rhotia kwa kujitoa katika kutekeleza shughuli za maendeleo. Amesema Zahanati ya Kainam Rhotia itakapokamilika itasaidi kusogeza huduma za afya karibu zaidi. Ameomba uongozi wa kijiji cha Kainam Rhotia kuweka nguvu katika ujenzi wa  zahanati ili uweze kukamilika kwa wakati.


Mh. Abbas Kayanda akikagua maendeleo ya ujenzi wa choo katika zahanati ya Kainam Rhotia

Matangazo

  • Matokeo ya upimaji wa Kitaifa kidoto cha pili January 07, 2024
  • Halmashauri ya Wilaya ya Karatu Uchaguzi wa Wanafunzi wa kidato cha kwanza, 2024 December 18, 2023
  • Matokeo ya Darasa la Nne January 07, 2024
  • KIKAO CHA BARAZA LA MADIWANI 2024 May 11, 2024
  • Angalia Zote

Taarifa Mpya

  • MAAFISA UANDIKISHAJI WALA KIAPO KARATU

    May 14, 2025
  • DED HOKORORO ASHIRIKI KIKAO CHA ALAT WILAYA YA MERU

    May 15, 2025
  • MADAKTARI BINGWA WA SAMIA AWAMU YA TATU WATUA KARAU

    May 12, 2025
  • KARATU WASAPOTIJUHUDI ZA RAIS SAMIA WATANGAZA UTALII WA NDANI

    May 11, 2025
  • Angalia Zote

Video

DC KOLIMBA ATATUA KERO TARAFA YA EYASI KARATU
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fursa za Uwekezaji

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Wizara ya Fedha na Mipango
  • Jamvi la Habari
  • Tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karatu District Council

    Sanduku la Posta: P.O Box 190

    Simu: +255 272970648

    Simu ya Mkononi: 0754773947

    Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa