Kamati ya siasa wilaya ya Karatu imekagua kiwanda cha maziwa Ayalabe kujioenea uendelevu wa kiwanda na kupewa taarifa ya kiwanda hicho cha maziwa. Kamati hiyo ya siasa imebaini madeni yaliyokopwa kwa dhamana ya kiwanda hicho ndio chanzo cha kufa kwa kiwanda hicho.
Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi ndugu Lucian Akonay amesema kama hati ya kiwanda imepelekwa TIB inamaana kiwanda kitauzwa. Amesema kiwanda lazima kifufuliwe na kifanye kazi, amesema watu waliopata uongozi wa kiwanda cha maziwa ni watu wazawa wa Karatu. Ndugu Lucian amesema inaonesha kuna kukingiana kifua kwa baadhi ya watu; jambo linalofanya kiwanda hicho kufa, ameomba afisa ushirika kupeleka nyaraka zote zinazohusiana na ubadhrifu wa kiwanda hicho ili chama kichukue hatua zaidi kwa wahusika.
Ndugu Lucian Akonay akikagua moja ya mitambo katika kiwanda cha Ayalabe
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Karatu ndugu waziri Mourice amesema kuna uhusiano mkubwa wa wajumbe wa Saccoss ambao ndio wajumbe kwenye kiwanda. Anasema Saccoss ilitumia hati ya kiwanda kwenda kukopa benki na hata wadaiwa watu walioshitakiwa kuhusiana na sakata la kufa kwa ujenzi wa kiwanda hicho kesi yake ilishafutwa. Ndugu Waziri anasema kwa sababu watu wanaodaiwa ndio watu hao hao viongozi; kiwanda hakiwezi kufanya kazi, amesema pengine serikali ingechukua maamuzi ya kukichukua kiwanda kirudi serikalini au kipewe muwekezaji binafsi.
Afisa ushirika Kastuli Sikay amesema kiasi cha shilingi million 513 zilitumika katika za jenzi wa kiwanda cha maziwa Ayalabe, na million 500 nyingine zilizokopwa na Saccoss kupitia benki ya TIB kwa dhamana ya eneo la kiwanda na kiwanda chenyewe. Ndugu Kastul amesema kuna uhusiano wa karibu wa saccoss na kiwanda cha maziwa cha Ayalabe na wajumbe wa bodi ya kiwanda hicho walijinufaisha na mikopo iliyokopwa na Saccoss. Taarifa za watu waliokopa katika kiwanda zipo na madeni ya kila mnufaika wa mikopo ipo.
Naye Mwenyekiti wa zamani ndugu Yuda Morata anasema Mrajisi wa mkoa naye amechangia sana kwenye kuzorota kwa kiwanda hicho. Amesema kuna kampuni zilizochukua fedha katika Saccos pamoja na wadaiwa sugu na iliundwa kampuni ya kufuatilia madeni lakini hakuna matokeo chanya yaliyopatikana. Ndugu Yuda amesema baada ya bodi kuanza kushughulikia watu ili warejeshe madeni, ni watu walio na madeni madogo tu walioshughulikiwa lakini wale watu waliokopa mikopo na madeni makubwa wameachwa na hawafuatiliwi. Ndugu Yuda amesema yeye amekopa million 30 lakini anashangaa anadaiwa million 4 kama mkopo wa ndani.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa