• Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Complains |
Karatu District Council
Karatu District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dhamira na Dira
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Ujenzi
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
    • Vitengo
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
  • Madiwani
  • Miradi
    • TASAF
    • BOOST
  • Machapisho
    • Hali ya Uwekezaji
      • Business License Form
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Habari
    • Hotuba kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha

UWAJIBIKAJI WALETA MATOKEO CHANYA MBULUMBULU

Posted on: June 6th, 2020

Na Tegemeo Kastus 

Kazi zote zinazofanywa na watumishi wa umma ni utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi, kila mmoja awajibike mahali pa kazi. Kata ya Mbulumbulu mambo mengi yametekelezwa na bado yanaendelea kutekelezwa, tumefanya kazi za barabara kazi za afya na kazi za shule.

Hayo yamesemwa na Mh. Elias Simpa diwani wa kata ya Mbulumbu  kwenye  Mkutano wa mwisho wa robo  ya mwisho wa kamati ya maendeleo ya kata ya Mbulumbu (ward development committee) ambao umefanyika katika kijiji cha Sloham. Amesema licha ya jitihada hizo bado kuna miradi ambayo haijamalizika mathalani mradi wa bararabara unaoendelea kujengwa; ameomba viongozi wa kata wasipambane na watu pindi dosari itakapotokea bali watumie busara ya kuwasiliana na mratibu wa mradi wa utengenezaji wa barabara ya Mbulumbulu.

Maeneo ambayo yamebaki na hayawezi kufikiwa na wakala wa barabara  vijijini  watawasiliana na wadau ili wakusanye mafuta ili Greda iendelee kufanya kazi ya tengenezaji wa barabara. Mh. Simpa amesema wataanzia shule saidizi ya Kituma kuja makao makuu ya kata, ameomba  wadau kuendelea kuchangia mafuta ili maeneo yote korofi yakarabatiwe, ametoa rai kwa wananchi wa Mbulumbulu kuendelea kutunza miundo mbinu ya barabara, miundo mbinu ya shule na miundo mbinu ya afya.

Kwa upande wake Afisa tarafa  wa tarafa ya Mbulumbulu Ndg. Saitoti Zelothe amesema Mvua kubwa za masika na  ushoroba wa wanyama pori uliokatisha katika eneo la hifadhi ya barabara vimeathiri kwa kiasi kikubwa barabara za ndani ya kata ya kambi ya simba. Amesema uongozi wa serikali wa kata umefanya  mawasiliano na NCCA pamoja na watu wa PAMS ili waweze kusaidia eneo liloharibika ambalo lipo katika eneo la hifadhi kiasi cha km 3-4, ili liweze kupitika vizuri. 

wananchi wakifuatilia taarifa ya mkutano wa maendeleo ya kata Mbulumbulu

Ndg. Zelothe amesema wamepata mwitikio chanya kutoka kwa wadau na mpango uliopo ni kukarabati  barabara hizo za ndani zilizoharibika ili ziweze kupitika kwa urahisi. Amesema utekelezaji huo utafanyika kwa kuwaomba wakala wa barabara  vitendea kazi kutengeneza eneo hilo ambao mpaka sasa wako eneo la maradi wakifanya ukarabati wa barabara iliyotengewa na serikali kiasi cha million 308 kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya kijiji cha kambi ya simba Mpaka lositete.

Ndg.  Zelothe amesema Tarafa ya Mbulumbulu imefaidika na awamu zote za REA ila kuna changamoto za upatikanaji wa umeme  upande wa kijiji cha lositete. Mkandarasi  anaangalia upande sahihi wa kuchukua umeme kati ya Upper kitete au upande wa chini wa wilaya ya Monduli. Amesema mkandarasi tayari ameshaanza kusambaza nguzo katika eneo hilo na matarajio ni kwamba ndani ya muda mfupi nyaya zitawekwa. Amesema kuna wananchi wametoa kiasi cha 27000 kwa ajili ya kuunganishiwa umeme na bado hawajaunganishiwa, Ndg. Zelothe amesema  ameshawasiliana  na meneja wa tanesco ndani ya  wiki mbili tatizo litakuwa limeshatatuliwa.Ndg. Zelothe amesema kuna baadhi ya taasisi ambazo hazijaunganishiwa na umeme licha ya kwamba taasisi hizo zilishatolewa taarifa za awali, ameahidi kuendelea kufuatilia na kuweka msukumo ili taasisi hizo  zipate umeme.

Ndug. Zelothe amesema serikali ya awamu ya tano chini Mhe. Rais  Dkt. John Pombe Magufuli imeshatoa fedha kwa ajili kukamilisha miradi mbalimbali iliyokuwa imesahaulika kwa muda mrefu. Amesema kwa tarafa ya Mbulumbulu kulikuwa na mradi wa zahanati ya Kainam Rhotia, zahanati ya Kilimatembo na shule ya sekondari ya Upper kitete. Amesema yeye kama Afisa Tarafa jukumu lake kwa sasa ni kuhakikisha mradi unaendana na dhamani ya fedha iliyotolewa (value of money). Ndg. Zelothe amesema amejiwekea ratiba kila siku mchana lazima akague miradi miwili katika eneo lake la kazi ndio maana miradi mingi katika tarafa ya Mbulumbulu imeweza kukamilika ndani ya wakati.

Naye Afisa Mtendaji kata Ndg. Elikana Sulumbu amesema wakati akitoa taarifa ya utendaji kazi wa kata ya Mbulumbulu, wamepokea kero 531, kero zilizotatuliwa ni 529. Amesema katika kero hizo 529 kero za ndoa ni 18 kero za za fedha 126, kero za migogoro ya ardhi 119 na kero za kutelekeza watoto 63. Amesema watumishi na viongozi wa umma wamesaidia kutatua kero hizo kwa kiasi kikubwa, amesema hayo yamewezekana kutokana na kufanya kazi kwa kushirikiana. Amesema kasi ya watu kupeleka mashauri ya kesi mahakamani imepungua kwa kiasi cha 80% ameongeza kusema hata kiasi 20%  walioenda mahakamani walishinda kesi zao.

wananchi katika matukio tofauti kwenye mkutano wa maendeleo kata ya Mbulumbulu

Matangazo

  • Matokeo ya upimaji wa Kitaifa kidoto cha pili January 07, 2024
  • Halmashauri ya Wilaya ya Karatu Uchaguzi wa Wanafunzi wa kidato cha kwanza, 2024 December 18, 2023
  • Matokeo ya Darasa la Nne January 07, 2024
  • KIKAO CHA BARAZA LA MADIWANI 2024 May 11, 2024
  • Angalia Zote

Taarifa Mpya

  • MAAFISA UANDIKISHAJI WALA KIAPO KARATU

    May 14, 2025
  • DED HOKORORO ASHIRIKI KIKAO CHA ALAT WILAYA YA MERU

    May 15, 2025
  • MADAKTARI BINGWA WA SAMIA AWAMU YA TATU WATUA KARAU

    May 12, 2025
  • KARATU WASAPOTIJUHUDI ZA RAIS SAMIA WATANGAZA UTALII WA NDANI

    May 11, 2025
  • Angalia Zote

Video

DC KOLIMBA ATATUA KERO TARAFA YA EYASI KARATU
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fursa za Uwekezaji

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Wizara ya Fedha na Mipango
  • Jamvi la Habari
  • Tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karatu District Council

    Sanduku la Posta: P.O Box 190

    Simu: +255 272970648

    Simu ya Mkononi: 0754773947

    Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa