• Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Complains |
Karatu District Council
Karatu District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dhamira na Dira
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Ujenzi
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
    • Vitengo
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
  • Madiwani
  • Miradi
    • TASAF
    • BOOST
  • Machapisho
    • Hali ya Uwekezaji
      • Business License Form
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Habari
    • Hotuba kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha

WANANCHI WAUNGA MKONO MPANGO WA MATUMIZI BORA YA ARDHI

Posted on: June 8th, 2020

Na Tegemeo Kastus

Mpango wa matumizi bora ya ardhi hauna uhusiano na kuchukua( kunyang’anya) ardhi ya wananchi. Ni utaratibu wanaojiwekea wananchi wenyewe kupanga matumizi bora ya ardhi yao kutokana na shughuli za asili za eneo husika.

Mkuu wa wilaya ya Karatu Mh. Theresia mahongo amesema hayo wakati akizungumza na wananchi katika kitongoji cha Gidamilanda katka kijiji cha Dumechang. Ameomba wananchi wa kitongoji hicho kutoa taarifa kwake moja kwa moja kwa mtu yeyote anayefanya upotoshaji dhidi ya mpango wa matumizi bora ya ardhi.  Amesema watu wanaopotosha wanaturudisha nyuma badala ya kwenda mbele, mpango wa matumizi bora ya ardhi si wa afisa ardhi wala si mpango wa mkuu wa wilaya.

Amesema mpango wa matumizi bora ya ardhi umewekwa kwenye ilani ya chama cha mapinduzi kinachoongozwa na Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ambaye ndiye Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi.  Amesema mpango wa matumizi bora ya ardhi ulizinduliwa katika Mkoa wa manyara (babati) na waziri wa ardhi nyumba na makazi Mh. William Lukuvi.

Mpango wa matumizi bora ya ardhi unafanywa na wananchi wenyewe, amesema wananchi wataitishwa kwenye mkutano na watapanga matumizi ya ardhi katika eneo lao la kitongoji wao wenyewe. Mh. Mahongo amesema watu wanaongezeka lakini pia mifugo nayo inaongezeka, ukiangalia idadi ya watu waliopo kwenye kitongoji cha Gidamilanda kwa sasa si sawa na miaka ya nyuma amesema hata idadi ya mifugo pia inazidi kuongezeka. Amesema mpango wa matumizi bora ya ardhi ni kusaidia kutunza ardhi iliyopo ili iweze kutumika vizuri.

Amesema mpango huo unaweza kurekebishika amesema ikitokea kuna kitu cha ziada wananchi wanataka kiwe katika sehemu ya mpango wao wa ardhi, wanaitisha kikao wanajadiliana  namna ya kuweka  mipango yao vizuri. Ametoa onyo kwa watu watakao potosha  mpango wa matumizi ya ardhi amesema hata wavumilia kabisa.

Awali katika mkutano huo katibu tawala wa wilaya ya karatu ndg, Abbas Kayanda alizungumza changamoto za kitongoji cha Gidamilanda; amesema  kutokuwa na mpango wa matumizi bora ya ardhi kumesababisha watu kuendelea kuvamia maeneo kiholela. Amesema  kuwa na matumizi bora ya ardhi kutasaidia kuepuka uvamizi wa meneo katika eneo hilo, wananchi sasa wanapaswa kushiriki kwenye mikutano ili kujadili namna ya kuweka ardhi katika mpango wa matumizi bora ya ardhi.Amesema hata matukio ya wageni wanaotoka pembezoni mwa wilaya nyingine na kuvamia eneo lao yatakwisha kabisa  na  wananchi wa Gidamilanda watatumia ardhi yao kwa matumizi watakayojipangia wao wenyewe .

wananchi wakiwa katika mkutano katika shule ya msingi Gidamilanda

Afisa ardhi wa Halmashauri ya Karatu Ndg. Faraji Rushagama  amesema mpango wa matumizi bora ya ardhi ni swala la kisheria ambalo linafanywa na wananchi wenyewe. Amesema  mpango unahusisha shughuli za asili zinazofanywa  katika eneo husika. Amesema mpango unasaidia kufahamu ni kipi kinafanywa na kijiji au kitongoji na kinafanyika kwa namna gani ??  ili kiweze kuboreshwa, amesema matumizi ya eneo husika na kiasi cha ardhi kinachopaswa kutumika kinapangwa na wananchi wenyewe wa eneo husika.

Amesema zoezi hilo wataalamu watajadiliana, kuelekezana na watashauriana na wakijiji    au kitongoji  kwa kina ameongeza kusema kama kuna mashaka  na mtaalamu wa kupima wa wilaya  na katika eneo husika  kuna mtaalamu  aliyesajiliwa na anatambulika basi atachukuliwa  ili kusaidi zoezi la mpango wa matumizi bora ya ardhi.

Ndg. Rushagama amesema sheria ya ardhi ya kijiji imewapa wananchi mamlaka ya kusimamia ardhi ya kijiji ambayo inahusika na kuilinda pamoja na kuipanga. Ameomba wananchi kutoa ushirikiano na kutunga sheria ndogo ambazo hazitatumika kuwaumiza wananchi wao wenyewe.

Nao wananchi wa kitongoji cha Gidamilanda wamesema namna walivyopokea swala la mpango bora wa matumizi bora ya ardhi katika eneo lao. Ndg. Dawte mkazi wa eneo hilo amesema awali walipata taarifa kwamba moja ya eneo lao ambalo linatumika kwa shughuli za malisho ya mifugo lingechukuliwa na kutegwa kwa ajili ya hifadhi ya game resereve. Kutokana na elimu waliyopata katika mkutano huo  pamoja na ufafanuzi wa kina wa  Mkuu wa wilaya kwamba hakuna eneo la kitongoji litakalochukuliwa,  limewapa faraja wananchi wa Gidamilanda na mwitikio chanya juu ya mpango wa matumizi bora ya ardhi.

wananchi wakifuatilia agenda za mkutano.

Matangazo

  • Matokeo ya upimaji wa Kitaifa kidoto cha pili January 07, 2024
  • Halmashauri ya Wilaya ya Karatu Uchaguzi wa Wanafunzi wa kidato cha kwanza, 2024 December 18, 2023
  • Matokeo ya Darasa la Nne January 07, 2024
  • KIKAO CHA BARAZA LA MADIWANI 2024 May 11, 2024
  • Angalia Zote

Taarifa Mpya

  • MAAFISA UANDIKISHAJI WALA KIAPO KARATU

    May 14, 2025
  • DED HOKORORO ASHIRIKI KIKAO CHA ALAT WILAYA YA MERU

    May 15, 2025
  • MADAKTARI BINGWA WA SAMIA AWAMU YA TATU WATUA KARAU

    May 12, 2025
  • KARATU WASAPOTIJUHUDI ZA RAIS SAMIA WATANGAZA UTALII WA NDANI

    May 11, 2025
  • Angalia Zote

Video

DC KOLIMBA ATATUA KERO TARAFA YA EYASI KARATU
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fursa za Uwekezaji

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Wizara ya Fedha na Mipango
  • Jamvi la Habari
  • Tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karatu District Council

    Sanduku la Posta: P.O Box 190

    Simu: +255 272970648

    Simu ya Mkononi: 0754773947

    Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa