• Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Complains |
Karatu District Council
Karatu District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dhamira na Dira
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Ujenzi
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
    • Vitengo
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
  • Madiwani
  • Miradi
  • Machapisho
    • Hali ya Uwekezaji
      • Business License Form
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Habari
    • Hotuba kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha

BILLION 5 KUTOLEWA FIDIA, UTANUZI WA UWANJA WA NDEGE

Posted on: September 3rd, 2020

NA TEGEMEO KASTUS

Fidia kwa ajili ya wananchi waliopisha utanuzi wa uwanja wa ndege wa Manyara, Karatu ipo katika hatua za mwisho kukamilika kwake ili wananchi walipwe fedha zao. Kilichobakia ni taarifa ya uthamini kusainiwa ili kwenda kwa Mthamini Mkuu wa serikali Dodoma na baadae taarifa hiyo kupelekwa Tanroad.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa wilaya ya Karatu Mh. Abbas Kayanda katika mkutano wa hadhara katika kijiji cha Kilimamoja. Amesema serikali haina  dhamira ya  kuchelewesha malipo kwa wananchi, Mh.Kayanda amesema kabla ya mwaka huu kuisha wananchi watakuwa wameshalipwa fidia zao. kiasi cha billion tano kitatolewa na serikali kwa ajili ya kuwafidia wananchi. Lakini kabla ya fedha hizo kutoka kuna taratibu zinapaswa kufuatwa na zikamilike ili fedha hiyo ya fidia kwa wananchi iweze kutolewa, Mh. Kayanda ameomba wananchi kuvuta subira ili uwasilishaji wa taarifa ya uthamini ukamilike, amesema swala hilo analifuatilia kwa karibu hatua kwa hatua. Wakati huo huo Mh. Kayanda ametoa maelekezo mahususi kwa mtendaji wa kijiji cha chemchem kusitisha zoezi la ugawaji wa viwanja katika kijiji cha chemchem mpaka maelekezo mengine yatakapotolewa.

Mh. Abbas Kayanda akizungumza na wananchi wa kijiji cha kilimamoja.

Mh. Kayanda ametoa maelekezo mahususi pia kwa viongozi wa kijiji cha Kilimamoja kusimamia na kuhakikisha ujenzi wa machinjio ya Kilimamoja unakamilika tarehe 10 mwezi wa tisa kama walivyojipangia. Lakini kuhakikisha ujenzi wa jengo la machinjio unaendana na thamani ya fedha  iliyotolewa,  Halmashauri imetoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa machinjio ya Kilimamoja hivyo ni jukumu la viongozi kusimamia ujenzi wa machinjio na kukamilika. Huduma za kuchinja mifugo katika kijiji cha kilimamoja kwa sasa zinafanyika Makuyuni.

Sambamba na hilo Mh. Kayanda ametoa maelekezo mahususi kwa viongozi wa kijiji kusimamia ujenzi wa zahanati katika kijiji cha Kilimamoja ili baadae serikali iongeze nguvu za kumalizia.Wananchi wa  kijiji cha kilimamoja walishaanza ujenzi wa Msingi wa zahanati, amesema wananchi lazima wawe chachu ya kuibua miradi ya maendeleo na kuchangia shughuli za maendeleo.

Wananchi wa kijiji cha kilimamoja wakimsikilza Mkuu wa wilaya  ya Karatu Mh. AbbasKayanda ( aliyesimama kulia) akihutubia

Mh. Kayanda ameelekeza uongozi wa maji kijiji cha Kilimamoja kuhakikisha wananchi wanapata maji. Amesema viongozi wa maji wamepewa dhamana ya kusimamia na kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji katika maeneo yao bila usumbufu. Mh, kayanda ametoa wito kwa wananchi kulipa bili za maji kwa wakati ili kusaidia usambazaji wa huduma za maji. Fedha hizo husaidia viongozi wa maji kufanya ukarabati wa miundo mbinu pindi inapotokea hitilafu.

Matangazo

  • WALIOCHANGULIWA KIDATO CHA KWANZA - 2023, HALMASHAURI YA KARATU December 14, 2022
  • LAKE EYASI CULTURAL TOURISM PROGRAM NEW ENTRY FEE December 01, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI NAFASI YA MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA 111 NA MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA 11 May 07, 2021
  • Angalia Zote

Taarifa Mpya

  • MIAKA (61) YA UHURU MKUU WA WILAYA YA KARATU MHE DADI HORICE KOLIMBA AFUNGUA MDAHALO WA MAENDELEO WILAYA YA KARATU.

    December 09, 2022
  • MAADHIMISHO YA MIAKA 61 YA UHURU WA TANGANYIKA

    December 09, 2022
  • MAADHIMISHO YA MIAKA 61 YA UHURU WA TANGANYIKA

    December 09, 2022
  • LAKE EYASI CULTURAL TOURISM TO BE IMPROVED

    November 08, 2022
  • Angalia Zote

Video

NDUGU. EDWARD MAURA MWENYEKITI WA BARAZA LA WAFUGAJI NGORONGORO
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fursa za Uwekezaji

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Wizara ya Fedha na Mipango
  • Tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karatu District Council

    Sanduku la Posta: P.O Box 190

    Simu: +255 272970648

    Simu ya Mkononi: 0754266833

    Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa