• Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Complains |
Karatu District Council
Karatu District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dhamira na Dira
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Ujenzi
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
    • Vitengo
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
  • Madiwani
  • Miradi
    • TASAF
    • BOOST
  • Machapisho
    • Hali ya Uwekezaji
      • Business License Form
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Habari
    • Hotuba kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha

KILIMO NA UFUGAJI WA KISASA, UNALIPA

Posted on: May 26th, 2021

wananchi wanapaswa kuanza kufanya kilimo na ufugaji wenye tija. Namna bora ya kukabiliana na changamoto za wafugaji na wakulima ni kutafuta mbinu shirikishi  zitakazohusisha wadau katika utatuzi, ili kuendelea kuongeza uzalishaji. Wadau wa kilimo na ufugaji wanahitaji  kuunganisha nguvu kwa pamoja badala ya kumuachia mkulima na mfugaji kuhangaika na utatuzi mwenyewe.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa wilaya ya Karatu Mh. Abbas Kayanda katika ziara ya siku ya pili kutembelea wakulima na wafugaji katika kijiji cha Chemchem, kujionea miradi ya shirika lisilo la serikali la Food for his children linavyosaidia kuimarisha familia duni kuweza kujikwamua kiuchumi. Amepongeza jitihada zinazofanywa na shirika hilo kwa wananchi wa Karatu, hasa kwa mafanikio ya dhahiri yaliyojikita katika ufugaji wa mbuzi wa kisasa aina ya sane. Lakini kwa namna wananchi walivyopokea miradi hiyo na kuona kama ni miradi ambayo inagusa maisha yao.

Mh. Abbas Kayanda akiwa anatoka kukagua zizi la mbuzi

Mh. Kayanda amesema changamoto kubwa ya ufugaji wa kisasa ni malisho ya mifugo ambayo kama ikitatuliwa  itamsaidia mfugaji kupata maziwa kwa wingi. Ametoa rai kwa shirika la Food for his children kuona namna ya kuja na mbinu shirikishi ili kumkwamua mfugaji hasa katika adha ya kupata malisho ya mifugo. Amesema kama mbuzi mmoja wa kisasa kwa makadirio ya juu akitunzwa vizuri anaweza kutoa lita tano kwa siku kwa maana ya kukamuliwa mara mbili asubuhi na jioni. Basi ipo haja ya shirika kukaa na wafugaji ili kuja na ufumbuzi wa changamoto zao kwa pamoja ili mwananchi aweze kunufaika zaidia na ufugaji.

Mh. Kayanda ameshauri shirika la Food for his children kupata takwimu sahihi za wananchi waliojihusisha na mradi huo. Amesema kupata takwimu za namna mbuzi wanavyozaliana lakini pia kupata takwimu za kiasi cha mbuzi waliouzwa. Amesema takwimu ndio ziatakazosaidia kujua mafanikio ya mradi na udhaifu wa mradi. Ameongeza kusema kuwa katika taarifa zao ni vyema wakawa na wasifu za mfugaji mmoja mmoja lengo likiwa ni kufahamu matokeo ya mradi kwa ujumla na matokeo ya mradi kwa mwananchi mmoja mmoja.

Mh.Abbas Kayanda akiwa anazungumza na mfugaji wa mbuzi

Meneja wa mradi Bi, Honorina Honorati amesema mbuzi wa kisasa wanaosambazwa na shirika la Food for his children, wanatabia ya kuzaa mapacha isipokuwa tu kwa uzazi wa kwanza. Ameongeza kusema mbuzi hao wanaweza kuzaa mara mbili kwa mwaka hivyo kumfanya mfugaji kuongeza idadi ya mbuzi lakini kufaidika na maziwa ya mbuzi.

Bi, Honorati amesema wafugaji wengi wa mbuzi wananufaika kwa biashara ya kuuza mabeberu ambao wanauza mpaka kiasi cha shilingi 200,000 kulingana na ukubwa na uzito. Amesema matarajio ya mradi ni kuona watu wengi wanafanikiwa, na wanapenda kujihusisha kaitika ufugaji wa mbuzi wa kisasa. Ili kutoa fursa kwa watu wengine wasioujua mradi kufundishwa na kuelewa misingi ya mradi.

Mama fabiola, Mfugaji wa mbuzi wa kisasa katika kijij cha Chemchem amesema kitu kinacholeta faraja katika mradi huo ni upatikanaji wa maziwa ambao unawawezesha kupata kipatao. Amesema katika miradi yake ya ujenzi hutegemea kuuza mabeberu ambao wamekuwa na soko kubwa. Amesema katika kijiji Chemchem changamoto kubwa wanayopata wafugaji ni fisi ambao wananyemelea mifugo yao wakati wa usiku.

Mh. Abbas kayanda akiwa katika matukio tofauti Kijiji cha Chemchem alipokuwa akitembelea miradi ya shirika la Food for his children


Matangazo

  • Matokeo ya upimaji wa Kitaifa kidoto cha pili January 07, 2024
  • Halmashauri ya Wilaya ya Karatu Uchaguzi wa Wanafunzi wa kidato cha kwanza, 2024 December 18, 2023
  • Matokeo ya Darasa la Nne January 07, 2024
  • KIKAO CHA BARAZA LA MADIWANI 2024 May 11, 2024
  • Angalia Zote

Taarifa Mpya

  • MAAFISA UANDIKISHAJI WALA KIAPO KARATU

    May 14, 2025
  • DED HOKORORO ASHIRIKI KIKAO CHA ALAT WILAYA YA MERU

    May 15, 2025
  • MADAKTARI BINGWA WA SAMIA AWAMU YA TATU WATUA KARAU

    May 12, 2025
  • KARATU WASAPOTIJUHUDI ZA RAIS SAMIA WATANGAZA UTALII WA NDANI

    May 11, 2025
  • Angalia Zote

Video

DC KOLIMBA ATATUA KERO TARAFA YA EYASI KARATU
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fursa za Uwekezaji

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Wizara ya Fedha na Mipango
  • Jamvi la Habari
  • Tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karatu District Council

    Sanduku la Posta: P.O Box 190

    Simu: +255 272970648

    Simu ya Mkononi: 0754773947

    Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa