• Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Complains |
Karatu District Council
Karatu District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dhamira na Dira
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Ujenzi
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
    • Vitengo
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
  • Madiwani
  • Miradi
    • TASAF
    • BOOST
  • Machapisho
    • Hali ya Uwekezaji
      • Business License Form
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Habari
    • Hotuba kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha

MBEGU ZA NGANO ZAINGIA KARATU

Posted on: March 10th, 2021

Na Tegemeo Kastus

Mbegu za ngano tani elfu kumi na saba imetolewa kwa wakulima waliojiunga katika vyama mbalimbali vya ushirika. Mbegu hizo ambazo zimeletwa na wakala wa mbegu za mazao mchanganyiko kanda ya kaskazini zinatarajiwa kupandwa msimu huu wa kilimo.

Hayo yamesemwa na Katibu tawala wa wilaya ya Karatu Bi. Faraja Msigwa alipokuwa akiwakabidhi wakulima wa ngano Rhotia Kati kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Karatu. Amesema ni wakati wa wakulima wa ngano kuanza kuwekeza katika kilimo cha ngano kwa kufuata mbinu za kilimo cha kisasa, ambazo zimetolewa kwa wakulima kabla ya kuletewa  mbegu za ngano.

Bi, Msigwa amesema bado kuna tani elfu thelathini na saba zinazotarajiwa kuletwa ili kuendana na mahitaji ya wakulima waliojiunga katika vyama vya ushirika. Ameomba wakulima wa ngano kuheshimu mikataba walioingia na wakala wa mbegu kanda ya kaskazini kupitia vyama vya ushirika ili kuondoa malalaniko wakati wa kuuza ngano. Amesema wakulima wanapaswa kuzalisha ngano yenye ubora inayoendana na mahitaji ya soko, kufanya hivyo itasaidia kukuza na kuimarisha soko la ndani la ngano.

Bi, Faraja Msigwa (kushoto) akikabidhi mbegu za ngano kwa wakulima Rhotia kati

Bi, Msigwa amesema mbegu zilizotoletwa na wakala wa mbegu mchanganyiko, kama mkulima ataweza kufuata masharti ya kilmo cha kisasa kwa hekari moja kuna uwezekano wa kupata gunia 25. Hayo yakiwa ni makadirio ya kiwango cha juu kwa uzalishaji na kiwango cha chini cha uzalishaji ni gunia 12, Bi, Msigwa amechukua nafasi hiyo kuishukuru serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mh. Dkt. John Pombe Magufuli kwa jitihada zinazofanywa katika kuboresha kilimo cha ngano.

Naye meneja wa mazao mchanganyiko kanda ya kaskazini Ndg. Hiza Kiluwasha amesema mbegu zilizoletwa ni mbegu ambazo zimekidhi kiwango, amesema mbegu hizo zimeletwa kupitia wakala wa mbegu seed Co. ameongeza kusema wakulima wakivuna mazao yao yatanunuliwa moja kwa moja na wakala wa mazao mchanganyiko ambao watainunua ngano yote.

Amesema wakala wa mazao mchanganyiko amesema watakuwa pamoja na wakulima wakati wa kuliandaa shamba wakati wa upandaji na wakati wa kuvuna. Ndg. Kiluwasha ametoa rai kwa wakulima kuacha kuchanganya mbegu za ngano wakati wa kulima kwa sababu watakuwa wamevunja masharti ya mkataba na ngano yao haitanunuliwa na wakala wa mazao mchanganyiko. Amesema mbegu za miche ya ngano zilizoletwa zina ubora unaoendana na mahitaji ya soko la ngano.

Wakala wa mazao mchanaganyiko ndg. Kiluwasha amesema wakulima walioingia kwenye mkataba ndio watakaonufaika na tani elfu 54. Amesema watafanya ufutiliaji wa kila mkulima shambani kwake kulingana na kiasi cha mbegu alichoomba ili kuondoa vitendo vya udanganyifu vinavyoweza kufanywa wakati wa ugawaji wa mbegu.

Bi, Faraja Msigwa akizungumza na wakulima wa ngano katika ofisi ya kijiji cha Rhotia kati.

Shehena ya mbegu za ngano iliyowasili katika ghala la kijiji Rhotia kati

Matangazo

  • Matokeo ya upimaji wa Kitaifa kidoto cha pili January 07, 2024
  • Halmashauri ya Wilaya ya Karatu Uchaguzi wa Wanafunzi wa kidato cha kwanza, 2024 December 18, 2023
  • Matokeo ya Darasa la Nne January 07, 2024
  • KIKAO CHA BARAZA LA MADIWANI 2024 May 11, 2024
  • Angalia Zote

Taarifa Mpya

  • MAAFISA UANDIKISHAJI WALA KIAPO KARATU

    May 14, 2025
  • DED HOKORORO ASHIRIKI KIKAO CHA ALAT WILAYA YA MERU

    May 15, 2025
  • MADAKTARI BINGWA WA SAMIA AWAMU YA TATU WATUA KARAU

    May 12, 2025
  • KARATU WASAPOTIJUHUDI ZA RAIS SAMIA WATANGAZA UTALII WA NDANI

    May 11, 2025
  • Angalia Zote

Video

DC KOLIMBA ATATUA KERO TARAFA YA EYASI KARATU
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fursa za Uwekezaji

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Wizara ya Fedha na Mipango
  • Jamvi la Habari
  • Tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karatu District Council

    Sanduku la Posta: P.O Box 190

    Simu: +255 272970648

    Simu ya Mkononi: 0754773947

    Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa