• Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Complains |
Karatu District Council
Karatu District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dhamira na Dira
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Ujenzi
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
    • Vitengo
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
  • Madiwani
  • Miradi
    • TASAF
    • BOOST
  • Machapisho
    • Hali ya Uwekezaji
      • Business License Form
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Habari
    • Hotuba kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha

MIRADI MMOJA WA TASAF MIKONONI MWA-TAKUKURU

Posted on: August 29th, 2020

NA TEGEMEO KASTUS

Mradi wa ujenzi wa choo cha shule ya msingi Bashay uliojengwa kwa nguvu za wananchi na Zahanati ya Bashay inayoendelea kujengwa na TASAF itachunguzwa na taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa. Ili kujiridhisha kama fedha zilizotolewa kwa ajili ya ujenzi wa  Miradi hiyo zinaendana na thamani ya ujenzi wa majengo yaliyojengwa.

Mh. Abbas Kayanda akikagua mradi wa ujenzi shule ya msingi Bashay

Maelekezo hayo yametolewa na Mkuu wa wilaya ya Karatu Mh. Abbas Kayanda aliyeambatana na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama, alipotembelea kujionea maendeleo ya ujenzi wa miradi hiyo. Mh. Kayanda ameoneshwa kutoridhishwa na umaliziaji wa ujenzi wa mradi wa zahanati ya Bashay kwa fedha ambazo zimetolewa na Tassaf. Licha ya uchunguzi kufanyika Mh. Kayanda amemuelekeza fundi anayesimamia ujenzi wa zahanati hiyo kuhakikisha dosari zilizojitokeza katika umaliziaji wa ujenzi wa mradi huo anazirekebisha kwa gharama zake. Ikiwa ni pamoja na kuhakikisha ujenzi wa mradi huo unakamilika na kuukabidhi kwa mujibu wa makubaliano tarehe 19 mwezi wa tisa. Mh. Kayanda ameelekeza ujenzi wa  jengo la mama na mtoto uanze haraka, ujenzi wa jengo la mama na mtoto katika zahanati hiyo utajengwa kwa nguvu za wananchi.

Mh. Abbas Kayanda akikagua ujenzi wa zahanati ya Bashay

Mh. Kayanda ametembelea na kujionea ujenzi wa choo cha matundu 12 katika shule ya Msingi Bashay ambao umegharimu takribani million tisa. Mh. Kayanda ameonesha kutoridhishwa na thamani ya ujenzi wa jengo hilo ukilinganisha na kiasi cha fedha kilichotolewa kwa ajili ya ujenzi. Sambamba na mradi huo wa ujenzi Mh. Kayanda ametembelea eneo linalotarajiwa kujengwa Vyumba viwili vya madarasa kwa fedha zilizotolewa na serikali kupitia mfuko wa EP4R. Ujenzi wa madarasa hayo unatarajiwa  kukamilika ndani ya kipindi cha siku 90, Mh. Kayanda ametoa rai kwa watendaji kusimamia vizuri ujenzi wa madarasa hayo kwa kuzingatia muda uliowekwa na lakini kuhakikisha ujenzi wa majengo hayo unaendana na thamani ya fedha zilizotolewa.

Mh. Abbas Kayanda ametembelea na kukutana na wajumbe wa kamati ya ujenzi wa zahanati ya Sumawe

Wakati huo huo Mh. Kayanda ametembelea ujenzi wa zahanati ya Sumawe ambayo ujenzi wake ulianza tangu mwaka 2011. Ameelekeza watendaji wa kuhakikisha ujenzi wa jengo la zahanati pamoja na ujenzi wa choo unakamilika ifikapo tarehe 30 mwezi wa tisa. Mh. Kayanda amemuelekeza Mganga mkuu wa wilaya kuhakikisha anaanda watumishi wa afya wa kuwapelekeka zahanati Sumawe pamoja na zahanati ya Bashay ili wananchi waanze kupata huduma za afya karibu na maeneo yao wanayoishi. Lengo likiwa ni kuondoa kadhia ya wananchi kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya.

Matangazo

  • Matokeo ya upimaji wa Kitaifa kidoto cha pili January 07, 2024
  • Halmashauri ya Wilaya ya Karatu Uchaguzi wa Wanafunzi wa kidato cha kwanza, 2024 December 18, 2023
  • Matokeo ya Darasa la Nne January 07, 2024
  • NAFASI ZA KAZI 2024 April 21, 2024
  • Angalia Zote

Taarifa Mpya

  • MILIONI 400 ZATOLEWA KARATU, KUJENGA MABWENI NA MADARASA EYASI SEKONDARI

    January 30, 2025
  • WASIMAMIZI WAASWA KUSIMAMIA VIAPO VYAO KUELEKEA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024.

    November 23, 2024
  • JESHI LA AKIBA MKAWE WAZALENDO KWA TAIFA

    November 23, 2024
  • HALMASHAURI YAZINDUA KITABU CHA MPANGO MKAKATI WA UKUSANYAJI MAPATO.

    November 19, 2024
  • Angalia Zote

Video

DC KOLIMBA ATATUA KERO TARAFA YA EYASI KARATU
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fursa za Uwekezaji

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Wizara ya Fedha na Mipango
  • Jamvi la Habari
  • Tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karatu District Council

    Sanduku la Posta: P.O Box 190

    Simu: +255 272970648

    Simu ya Mkononi: 0754773947

    Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa