• Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Complains |
Karatu District Council
Karatu District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dhamira na Dira
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Ujenzi
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
    • Vitengo
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
  • Madiwani
  • Miradi
    • TASAF
    • BOOST
  • Machapisho
    • Hali ya Uwekezaji
      • Business License Form
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Habari
    • Hotuba kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha

SEKTA YA AFYA HAWAPOI

Posted on: April 15th, 2021

Na Tegemeo Kastus

Hatuhitaji wakinamama watembee umbali mrefu kwenda kujifungua, tunataka miundo mbinu ya jengo la uzazi itengemae ili huduma za utoaji wa afya zizidi kuimarika.  Barabara hii ya Kainam Rhotia imekuwa na changamoto kipindi  cha masika, hivyo kuwa na zahanati yenye kutoa huduma bora za afya katika kijiji cha Kainam ni jambo la msingi.

Huduma za uzazi zitakuwa zinafanywa katika moja ya chumba katika zahanati ya Kainam Rhotia wakati upande wa jengo la zahanati wakati upande uliobakia ukiendelea kukamilishwa. Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya ya Karatu Mh. Abbas Kayanda alipokuwa akifungua zahanati ya Kainam Rhotia. Zahanati hiyo imechukua muda wa miaka 14 mpaka kufikia hatua ya kufunguliwa. Kituo hicho kimekamilika baada ya fedha kiasi cha million 6 zilizotolewa kwenye mfuko wa jimbo kutumika kwa ajili ya umaliziaji wa upande mmoja wa zahanati. Mh.Kayanda  amesema wakinama walikuwa wanatembea umbali wa km 7 kufuata huduma za afya katika kituo cha afya cha Rhotia kati, baada ya uzinduzi wa zahanati hiyo huduma za afya zitakuwa zinapatikana zahanati ya Kainam Rhotia.

Mh. Abbas Kayanda (katikati) akiwa katika chumba cha maabara katika zahanati ya Kainam, Rhotia

Mh. Kayanda amesema serikali imekuwa ikisimamia maswala ya afya katika maeneo mbalimbali; afya ni jambo la msingi, bila afya hatuwezi kufanya kazi kwa ufanisi bila afya huwezi kusoma hivyo ukiwa na afya ni mtaji wa kufanya shughuli za maendeleo. Amesema kuanzia sasa  chanjo ya polio itaanza kutolewa katika zahanati ya Kainam Rhotia, amehimiza wananchi wa kujiunga na mfuko wa bima ya afya iliyoboreshwa ili kukijengea uwezo kituo cha afya kiwe kinauwezo wa kujinunulia dawa.

Amesema zahanati lazima iwe na mgao wake wa dawa, ili kiweze kujijengea uwezo wa kauagiza dawa kulingana na mahiaji, katika swala la afya wakinamama na watoto ndio wahanga wakubwa. Tukijiunga na mfuko wa bima afya ya jamii unasaidia kupata huduma wakati wowote katika kipindi cha mwaka hata kama changamoto ya afya itakukuta katika kipindi ambacho huna  fedha kwa ajili ya kupata huduma za afya.Katika hatua nyingine Mh. Kayanda ameagiza uongozi wa kijiji cha Kainam Rhotia kuchagua wajumbe wa kamati ya zahanati  ya afya katika mkutano mkuu wa kijiji wa wiki ijayo. 

Naye muwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Karatu Mganga Mkuu wa wilaya ya Karatu Dkt. Lucas Kazingo amesema zahanati ya Kainam Rhotia imepata wahudum wa afya wawili na mtu wa maabara yuko mbioni kuja  kwa ajili kufanya kazi ya vipimo katika zahanati ya Kainam Rhotia. Dkt. Kazingo amesema wametenga chumba kimoja kwa ajili ya kutoa huduma za uzazi ili kuhakikisha hakuna mama mjamzito ana kosa huduma ya uzazi katika zahati wakati ujenzi ukiendelea katika jengo la mama na mtoto.

Mh. Abbas Kayanda akikagua jengo la zahanati ya Kainam Rhotia.

Katibu wa jumuiya ya umoja wa wanawake chama cha mapinduzi Bi, Maua Hasani amesema ilani ya chama ambayo inatekelezwa na serikali imejikita katika kuhakikisha kila kijiji kinakuwa na zahanati yake na kila kata  inakuwa na kituo cha afya  na kila wilaya kuwa na  hospitali ya wilaya. Amesema ziara ya kamati ya siasa iliyofanywa mwaka juzi 2019 ndio imewezesha zahanati hiyo kuanza kufanya kazi. Bi. Hasani ameomba wananchi kutovunjika moyo na badala yake waendelee kufanya shughuli zao za maendeleo.

Bi, Christina Lulu Mkazi wa kijiji cha Kainam Rhotia amesema wanaishukuru sana serikali kwa kulichukulia kwa uzito swala la ujenzi wa zahanati, Amesema wakinamama wanajukumu kubwa la kujali afya za watoto na familia kwa ujumla. Ameomba serikali isiishie kwenye kulizindua tu jengo la zahanati bali ihakikishe huduma zinaendelea kuimarika kadri siku zinavyosonga mbele. Bi, Lulu amesema wao kama kinamama na wananchi wa Kainam Rhotia wataendelea kushirikiana na serikali katika kila hatua ili kuleta maendeleo katika zahanati ya Kainam Rhotia.

Mh. Abbas kayanda akikata utepe kama ishara ya kuzindua jengo la zahanati ya Kainam Rhotia

Matangazo

  • Matokeo ya upimaji wa Kitaifa kidoto cha pili January 07, 2024
  • Halmashauri ya Wilaya ya Karatu Uchaguzi wa Wanafunzi wa kidato cha kwanza, 2024 December 18, 2023
  • Matokeo ya Darasa la Nne January 07, 2024
  • KIKAO CHA BARAZA LA MADIWANI 2024 May 11, 2024
  • Angalia Zote

Taarifa Mpya

  • MAAFISA UANDIKISHAJI WALA KIAPO KARATU

    May 14, 2025
  • DED HOKORORO ASHIRIKI KIKAO CHA ALAT WILAYA YA MERU

    May 15, 2025
  • MADAKTARI BINGWA WA SAMIA AWAMU YA TATU WATUA KARAU

    May 12, 2025
  • KARATU WASAPOTIJUHUDI ZA RAIS SAMIA WATANGAZA UTALII WA NDANI

    May 11, 2025
  • Angalia Zote

Video

DC KOLIMBA ATATUA KERO TARAFA YA EYASI KARATU
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fursa za Uwekezaji

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Wizara ya Fedha na Mipango
  • Jamvi la Habari
  • Tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karatu District Council

    Sanduku la Posta: P.O Box 190

    Simu: +255 272970648

    Simu ya Mkononi: 0754773947

    Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa