• Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Complains |
Karatu District Council
Karatu District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dhamira na Dira
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Ujenzi
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
    • Vitengo
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
  • Madiwani
  • Miradi
    • TASAF
    • BOOST
  • Machapisho
    • Hali ya Uwekezaji
      • Business License Form
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Habari
    • Hotuba kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha

SERIKALI KUSAKA FISI WANAO HATARISHA UHAI WA WATU BASODAWISH

Posted on: November 14th, 2020

NA TEGEMEO KASTUS

Kikosi kazi maalumu kitakachohusisha maaskari wa hifadhi ya ziwa Manyara (TANAPA) na Mamlaka ya Ngorongoro wakisaidiana maaskari wanyamapori wa Halmashauri ya Karatu watafanya kazi ya kusaka fisi anayekula watu  katika kata ya Endamarariek.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa wilaya ya  Karatu Mh. Abbas Kayanda wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara kijiji cha Basodawish. Amesema licha ya hatua zitakazochukuliwa na serikali za kumsaka fisi huyo ambaye anajitokeza katika mazingira ya kutatanisha na hali ng'ombe wala mbuzi anakula watoto wadogo.  Mh. Kayanda ametangaza siku  mbili za maombi kila kijiji katika kata hiyo ili kumuomba mwenyezi Mungu kuepusha janga hilo na siku ya tatu ya maombi yatafanyika Makao Makuu ya  kata  na yataongozwa na viongozi wa dini wa kata pamoja na Wilaya.

Mh. Kayanda amesema katika kijiji cha Basodawish yametokea matukio sita na matukio mawili yamegharimu uhai wa watu. Kijiji cha Shangt yametokea mashambulizi mawili kati ya hayo matukio watoto wawili walijeruhiwa na watoto wawili walifariki dunia. Katika kijiji cha Endamarariek limetokea tukio la mtoto kujeruhiwa na tukio jingine kugharimu uhai wa mtoto. Katika kijiji cha Gidbaso  liltokea tukio moja lakini hakuna mtoto aliyejeruhiwa. Amesema katika matukio kumi  jumla yaliyotokea tangu mwaka 2019 kati ya hayo matukio matatu yametokea  mwaka 2020  ambayo mawili ndio yamesababisha vifo na moja mtoto kujeruhiwa.

Mkuu wa wilaya ya Karatu Mh. Abbas Kayanda akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara kijiji cha Basodawish.

Wakati akifungua kikao hicho Mwenyekiti wa kijiji cha Basodawish Ndg. Meta Petro Bare amesema katika siku tatu fisi amekuwa hatare sana kwa uhai wa watu. Amesema kwa mtirirko wa matukio inaonekana ni fisi mmoja tu anayesumbua eneo zima la kata ya Endamarariek. Amesema tukio la juzi kuna mtoto aliyeng’atwa na fisi na kuna binti ambaye pia aling’atwa na fisi. Amesema hali ya binti inaendelea vizuri na ameruhusiwa kutoka hospital na mtoto aliyevamiwa na fisi amepelekwa katika kituo cha afya cha Fame na alikuwa katika hatua za kufanyiwa upasuaji.

Matangazo

  • Matokeo ya upimaji wa Kitaifa kidoto cha pili January 07, 2024
  • Halmashauri ya Wilaya ya Karatu Uchaguzi wa Wanafunzi wa kidato cha kwanza, 2024 December 18, 2023
  • Matokeo ya Darasa la Nne January 07, 2024
  • NAFASI ZA KAZI 2024 April 21, 2024
  • Angalia Zote

Taarifa Mpya

  • MILIONI 400 ZATOLEWA KARATU, KUJENGA MABWENI NA MADARASA EYASI SEKONDARI

    January 30, 2025
  • WASIMAMIZI WAASWA KUSIMAMIA VIAPO VYAO KUELEKEA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024.

    November 23, 2024
  • JESHI LA AKIBA MKAWE WAZALENDO KWA TAIFA

    November 23, 2024
  • HALMASHAURI YAZINDUA KITABU CHA MPANGO MKAKATI WA UKUSANYAJI MAPATO.

    November 19, 2024
  • Angalia Zote

Video

DC KOLIMBA ATATUA KERO TARAFA YA EYASI KARATU
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fursa za Uwekezaji

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Wizara ya Fedha na Mipango
  • Jamvi la Habari
  • Tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karatu District Council

    Sanduku la Posta: P.O Box 190

    Simu: +255 272970648

    Simu ya Mkononi: 0754773947

    Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa