NA TEGEMEO KASTUS
Viongozi wa dini waombwa kuweka mkazo katika kusimamia maadili ya jamii, ili kupunguza vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia pamoja na upotevu wa maadili ambavyo vimezidi kukithiri katika jamii.
Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya ya Karatu Mh. Abbas Kayanda wakati akifungua semina ya kamati ya umoja ya viongozi wa dini inter faith. Amesema serikali ina amini sana viongozi wa dini katika kujenga jamii yenye hofu ya Mungu. Amesema changamoto ya upotevu wa maadili inasababisha watoto kutaabika; na imeongeza watoto wanaoishi katika mazingira magumu, lazima tuwaambie na tuwabadilishe nafsi zao watu hawa, kwamba mambo wanayoyofanya hayampendezi mwenyezi Mungu.
Mkuu wa wilaya ya Karatu, Mh. Abbas Kayanda akizungumza na kamati ya umoja wa viongozi wa dini katika ukumbi wa KKKT Karatu
Mh. Kayanda amepongeza wazo la kuwa na kamati ya umoja wa viongozi wa dini (inter face) amesema umoja huo utasaidia serikali katika mazoezi ya kitaifa kama chanjo, kusaidia kuhamasisha wananchi. Umoja wa viongozi wa dini inter face utasadia kuleta wananchi pamoja. Sambamba na hayo Mh. Kayanda amewashukuru viongozi wa dini kwa kuombea amani ya nchi kipindi cha uchaguzi. Tumemaliza uchaguzi wetu salama hakuna vita wala hakuna ogomvi hili ni jambo la kujivunia. amesema uchaguzi Mkuu umeisha lazima wananchi tuungane na tuwe kitu kimoja na tushiriki katika shughuli za maendeleo. Maendeleo ya wanakaratu yataletwa na wana karatu wenyewe na si mtu nje ya Karatu.
Mh. Kayanda ameomba viongozi wa dini kuendelea kuhubiri amani na kuitunza, kwa sababu ndio msingi wa maendeleo ya nchi. Amesema amani ni tunu ya kipekee, hatuwezi kujenga hospitali kujenga barabara au kununua ndege kama amani itatetereka. Mh. Kayanda ametumia nafasi hiyo kupongeza kamati ya umoja wa viongozi wa dini inter face kwa miradi mbalimbali wanayosimamia kwa ajili ya kusaidia jamii.
Akitoa neno la shukrani Padre Pamphili Nada amesema viongozi wa dini wataendelea kuhubiri amani kwa kundi kubwa la waumini ambalo liko nyuma yao. Amesema lazima mwanadamu apate maendeleo ya kweli ya roho na mwili, amani ikitoweka basi hakuna kitakachowezekana. Tunashukuru Mungu tumepata Rais makini mwenye maono, ujasiri wake umetuvusha kwenye changamoto ya korona. Viongozi wa dini kwa pamoja wameahidi kuendelea kushirikiana na serikali wakati wowote.
Mkuu wa wilaya Mh. Abbas Kayanda akiwa katika picha ya pamoja na kamati ya umoja wa viongozi wa dini Karatu
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa