• Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Complains |
Karatu District Council
Karatu District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dhamira na Dira
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Ujenzi
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
    • Vitengo
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
  • Madiwani
  • Miradi
    • TASAF
    • BOOST
  • Machapisho
    • Hali ya Uwekezaji
      • Business License Form
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Habari
    • Hotuba kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha

ZAHANATI YA KILIMATEMBO MBIONI KUKAMILIKA

Posted on: August 16th, 2021

Na Tegemeo Kastus

Kasi ya umalizijaji ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Kilimatembo katika kata ya Rhotia imefika katika hatua za nzuri kukamilika. Zahanati hiyo ambayo ilitengewa kiasi cha million kumi na Halmashauri ya wilaya ya Karatu ikiwa ni pamoja na na fedha za kijiji kiasi cha Milion nne kutoka Halamashauri ya kijiji cha kilimatembo na nguvu kazi za wananchi sasa iko katika hatua za umaliziaji wa ujenzi wa kichomea taka na jengo la choo.

 Mh. Kayanda akizungumza na viongozi wa kijiji cha kilimatembo

Hayo yamebainika katika ziara ya Mkuu wa wilaya Mh. Abbas Kayanda wakati alipotembelea kujionea maendeleo ya ujenzi wa zahanati hiyo. Mh. Kayanda amepongeza jitihada zilizofanywa na wananchi pamoja na uongozi wa kijiji kwa usimamizi mzuri wa kazi ya ujenzi unaoendelea. Katika ziara hiyo Mh. Kayanda ameelekeza wakala wa barabara vijijini (Tarura) kuweka kwenye bajeti ya mwaka (2022-2023) ujenzi wa wa daraja katika barabara ya Rhotia-Marar ambayo mwaka huu iko katika mpango wa kuchongwa kwa umbali wa km 1. Amesema ujenzi wa daraja hilo utasaidia usalama wa wanafunzi kuvuka wakati wa kwenda shule lakini pia kusaidia wananchi kupata huduma ya afya katika zahanati ya Kilimatembo.

Mh. Kayanda akikagua ujenzi wa jengo la zahanati ya Kilimatembo.

Mh. Kayanda amesema vifaa vyote vya ujenzi vimeshaletwa katika zahanati hiyo ameelekeza wataalamu mpaka mwanzoni mwa mwezi wa kumi zahanati ianze kufanya kazi. Amemuelekeza Mganga mkuu wa wilaya kuanza kutafuta wafanyakazi wa afya watakaokuja kutoa huduma za afya kwa kwenye zahanati ya Kilimatembo.

Mh. Kayanda ameelekeza wakala wa barabara vijijini kuweka katika bajeti barabara ya kutoka kijiji cha Kilimatembo Mpaka kijiji cha Huduma ili iweze kujengwa na kupanuliwa kurahisisha mawasiliano ya barabara ya kijiji hicho. Akizungumzia kuhusu swala la maji amesema serikali  ya awamu ya sita inayoongozwa na Mh.  Samia Suluhu Hasani imetoa kiasi cha 2.2 billion kwa Ruwasa kwa ajili ya miradi ya maji ikiwemo  kiasi cha million 320 kwa ajili ya uboreshaji wa miundo mbinu ya maji katika kata ya Rhotia. Uboreshaji wa huduma za maji utasaidia maji kusambazwa mpaka kijiji cha Kilimatembo.

Mh. Kayanda katika matukio tofauti katika jengo la zahanati ya Kilimatembo

Katika hatua nyingine Mh. Kayanda ameelekeza shirika la umeme Tanesco (Karatu) kufanya upembuzi yakinifu kwenye miundo mbinu ya umeme ili kubainisha na kurekebisha tatizo la kijiji cha Kilimatembo kukosa nishati ya umeme yenye uwezo wa kuhimili vifaa vya umeme wa manyumbani na mashine za kusagia. Amesema malengo ya serikali kufikia mwaka 2025 ni kusambaza umeme mpaka ngazi ya vitongoji baada ya kumaliza ngazi ya kijiji. Amesema ujenzi wa miundo mbinu ya umeme unatakiwa uwe na  faida kwa wananchi kama  kuwezesha shughuli za kiuchumi na kusaidia katika miradi ya maendeleo.

Mh. Kayanda amehimiza wananchi walijitokeza katika hadhara hiyo umuhimu wa kujiunga katika vikundi ili kuanzisha mradi wa kutundika mizinga ya  nyuki katika maeneo ya fireline ambayo huvamiwa na wanyama pori.  Amesema  kutundika mizinga ya nyuki mipakani mwa hifadhi ya wanayama inasaidia tembo kutoingia kwenye  makazi ya watu lakini inasaidia wananchi kujipatia kipato kutokana na asali wanayorina na kuuza. Amesema mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro imeanzisha ufugaji wa nyuki wa vikundi na tayari vikundi 23 vimeshapewa mizinga kwa ajili ya uanzishaji wa mradi huo. Tayari mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro wanampango wa kujenga kiwanda kwa ajili ya utengenzaji wa asali ambacho kitasaidia kuiongezea asali thamani ya fedha.

Mh. Kayanda akiwa katika ziara ya kukagua miundo mbinu ya ujenzi ya elimu sekondari ya Diego.

Amesema mamlaka imekuwa na ikitumia vijana waliopewa mafunzo (Game scout) ambao wanatoka katika vijiji vinavyozunguka hifadhi ya mamlaka Ngorongoro ili kusaidia kurudisha wanyama wanaoingia kwenye makazi ya watu. Ikiwa na pamoja na kupaka oil chafu na pilipili ambayo inasadia sana wanayama mwitu kutoingia kwenye makazi ya watu, amesema sambamba na hilo vijana hao wanasaidia kutoa taarifa mbalimbali katika vituo vya ulinzi vya hifadhi kusaidia kukabiliana na vitendo vya kijangili

Awali katika ziara hiyo Mh. Abbas Kayanda alitembelea shule ya sekondari Diego na Kilimatembo kujionea hatua za ujenzi wa vyoo katika shule hizo. Mh. Kayanda amehimiza watendaji kuongeza nguvu kazi ili miradi ya ujenzi wa vyoo katika shule hizo ili viweze kukamilika kwa wakati. Ujenzi wa wa matundu ya vyoo uko katika hatua za mwisho na kilichaobaki ni ukarabati wa mdogo mdogo ambao uko katika hatua nzuri.

Picha katia matukio tofauti wakati wa ziara ya kukagua miundo mbinu ya elimu katika shule ya sekondari Kilimatembo.

Matangazo

  • Matokeo ya upimaji wa Kitaifa kidoto cha pili January 07, 2024
  • Halmashauri ya Wilaya ya Karatu Uchaguzi wa Wanafunzi wa kidato cha kwanza, 2024 December 18, 2023
  • Matokeo ya Darasa la Nne January 07, 2024
  • NAFASI ZA KAZI 2024 April 21, 2024
  • Angalia Zote

Taarifa Mpya

  • MILIONI 400 ZATOLEWA KARATU, KUJENGA MABWENI NA MADARASA EYASI SEKONDARI

    January 30, 2025
  • WASIMAMIZI WAASWA KUSIMAMIA VIAPO VYAO KUELEKEA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024.

    November 23, 2024
  • JESHI LA AKIBA MKAWE WAZALENDO KWA TAIFA

    November 23, 2024
  • HALMASHAURI YAZINDUA KITABU CHA MPANGO MKAKATI WA UKUSANYAJI MAPATO.

    November 19, 2024
  • Angalia Zote

Video

DC KOLIMBA ATATUA KERO TARAFA YA EYASI KARATU
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fursa za Uwekezaji

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Wizara ya Fedha na Mipango
  • Jamvi la Habari
  • Tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karatu District Council

    Sanduku la Posta: P.O Box 190

    Simu: +255 272970648

    Simu ya Mkononi: 0754773947

    Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa