• Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Complains |
Karatu District Council
Karatu District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dhamira na Dira
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Ujenzi
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
    • Vitengo
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
  • Madiwani
  • Miradi
    • TASAF
    • BOOST
  • Machapisho
    • Hali ya Uwekezaji
      • Business License Form
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Habari
    • Hotuba kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha

FUATENI MAELEKEZO YA WIZARA YA AFYA!! WAKATI WA UBORESHAJI

Posted on: April 15th, 2020

Na Tegemeo Kastus

Katibu Tawala wa wilaya ya Karatu Ndg. Abbas Kayanda amehimiza Maafisa waandikishaji na BVR KIT OPERATORS kuchukua tahadhari inayotolewa na wizara ya afya, wakati huu wa ugonjwa wa virusi vya corona kwenye zoezi la uboreshaji daftari la wapiga kura.

Ndg. Kayanda amesema ni vizuri tahadhari zote zikachukuliwa vizuri ili zoezi la uandikishaji lisiwe chanzo cha kueneza ugonjwa. Amesema hayo wakati akihitimisha semina ya siku moja ya maafisa wandikshaji na BVR operators katika ukumbi wa Afisa tarafa Karatu. Zoezi la maboresho ya daftari la wapiga kura linatarajiwa kuanza 17/4/2020 na kufanyika kwa muda wa siku tatu.

Ndg. Kayanda amesema zoezi linahitaji uvumilivu na umakini mkubwa katika ujazaji wa taarifa, ametoa wito asingependa kuona wilaya ya Karatu inakuwa na dosari yeyote katika zoezi la maboresho ya daftari la wapiga kura. Amesema waandikishaji na Bvr Operators wamepewa dhamana kufanya kazi kwa niaba ya watu wengine, isingekuwa rahisi wote sisi katika wilaya ya Karatu tushiriki katika zoezi kama hilo. Hivyo waandikishaji wamechaguliwa kwa sababu wanaaminika na wataitendea haki kazi walioyopewa.

Kwenye vikao vya tathimini juu ya kazi ya uboreshaji wa daftari la wapiga kura, wilaya ya Karatu iwe kinara kwa kufanya vizuri katika zoezi hilo. Ameomba wataalamu kutoa maelekezo mazuri ya ufasaha kwa watendaji wa chini ili kazi iweze kwenda vizuri. Ndg, Kayanda ametoa wito kwa watendaji watakao kabidhiwa vifaa kuvitunza vizuri. Amesema zile mashine za BVR KIT ni  mashine za gharama kubwa na madhumuni ni kufanya uchaguzi kwa njia za kisasa. Ameomba wandikishaji kutunza mashine kwa kuhifadhi vizuri lakini pia kuzitunza kwa kuzitumia vizuri. Ndg. Kayanda amewataka watendaji vijiji na kata kuhamasisha wananchi kujitokeza na kuboresha taarifa katika dafatari la wapiga kura.

Awali Ndg. Waziri Mourice Afisa Mwandikishaji wa wilaya ya Karatu, amesema kuna uwezekano watu wengi wakajitokeza katika uboreshaji wa daftari la wapiga kura  kwa sababu vyuo na shule zimefungwa. Ameomba Maafisa waandikishaji kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa ili kuweza kutimiza malengo.

Ndg. Waziri amesema mawakala wa vyama vya siasa ni watazamaji lakini siyo watoa maelekezo katika zoezi hilo. Amesema jambo lolote la dharura litakalojitokeza, waandikishaji watoe taarifa kwa watendaji wa kata ili waweze kutatua changamoto zitakazojitokeza katika zoezi.   

Ndg. Waziri amesema katika zoezi hilo, wananchi watakuja vituoni na watataka kuelimishwa namna ya kuboresha taarifa zao katika daftari la wapiga kura. Ameombwa waandikishaji kutumia busara kuwaelekeza wananchi kwa upole ili zoezi liende vizuri. Amesema ndio maana tume ya taifa ya uchaguzi inafanya mafunzo mara kwa mara kwa wataalamu ili kukumbusha watendaji na kuongeza ufanisi katika utendaji wa kazi kwa sababu binadamu tumeumbiwa kusahau.

Matangazo

  • Matokeo ya upimaji wa Kitaifa kidoto cha pili January 07, 2024
  • Halmashauri ya Wilaya ya Karatu Uchaguzi wa Wanafunzi wa kidato cha kwanza, 2024 December 18, 2023
  • Matokeo ya Darasa la Nne January 07, 2024
  • KIKAO CHA BARAZA LA MADIWANI 2024 May 11, 2024
  • Angalia Zote

Taarifa Mpya

  • MAAFISA UANDIKISHAJI WALA KIAPO KARATU

    May 14, 2025
  • DED HOKORORO ASHIRIKI KIKAO CHA ALAT WILAYA YA MERU

    May 15, 2025
  • MADAKTARI BINGWA WA SAMIA AWAMU YA TATU WATUA KARAU

    May 12, 2025
  • KARATU WASAPOTIJUHUDI ZA RAIS SAMIA WATANGAZA UTALII WA NDANI

    May 11, 2025
  • Angalia Zote

Video

DC KOLIMBA ATATUA KERO TARAFA YA EYASI KARATU
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fursa za Uwekezaji

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Wizara ya Fedha na Mipango
  • Jamvi la Habari
  • Tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karatu District Council

    Sanduku la Posta: P.O Box 190

    Simu: +255 272970648

    Simu ya Mkononi: 0754773947

    Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa