Jumuiya ya Tawala za Mitaa Mkoa wa Arusha (ALAT) imefanya ziara ya Kukagua Miradi ya Maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya Meru na Kupongeza Juhudi za Serikali katika ujenzi na uboreshaji wa Miradi hiyo.
Jumuiya hiyo iliyoongozwa na Mwenyekiti wake Ambae ni Meya wa Jini la Arusha Mhe. Maxmillian Iranghe imetembelea miradi mbalimbali ikiwemo miradi ya Elimu, Afya na Miradi mingine inayotekelezwa kwa Fedha za Ndani ikiwemo Uzio wa Soko.
Akizungumza Mwenyekiti Iranghe Baada ya Ukaguzi wa Miradi ameipongeza Halmashauri ya Meru kwa kusimamia vyema fedha za serikali na kukamilisha miradi hiyo tajika katika jamii.
Kwa Upande wake Katibu wa Jumuiya hiyo ya ALAT Ndg. Juma Hokororo ambae ni Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu kwa niaba ya Jumuiya hiyo amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassn kwa kutoa fedha za kutosha za miradi katika mkoa mzima wa Arusha.
Amesema ni wajibu wao kama wakurugenzi kwa kushirikiana na Wenyeviti wa Halmashauri na madiwani pamoja na viongozi wengine kushikamana na kusimamia miradi hiyo ikamilike na kuhakikisha inatoa huduma husika kwa ubora ulio nuiwa.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa