MAJUKUMU YA IDARA YA ELIMU YA MSINGI
1. Kusimamia utekelezaji wa usimamizi wa mtaala wa Elimu Msingi
2. Kusimamia utendaji wa kazi za walimu katika ujifunzaji na ufundishaji
3.kusimamia utunzaji na uboreshaji wa miundo mbinu ya shule kama madarasa, nyumba za walimu, vyoo na ofisi za walimu.
4:Kusimamia rasilimali fedha na utekelezaji wa bajeti za shule.
5:Kuhakikisha kunakuwepo na ustawi wa walimu na wanafunzi katika maeneo ya kazi.
6:Kudumisha ushirikiano baina ya shule na wadau mbalimbali katika kuleta maendeleo ya shule.
7:Kuhakikisha shule zote zinakuwa na samani kwa walimu na wanafunzi kama madawati, meza kabati nk.
8:Kuhakikisha mazingira ya shule yanatunzwa na yanavutia
9:Kuhakikisha kila mwanafunzi mwenye umri wa kwenda shule anaandikishwa na anapata masomo.
10:Kuhakikisha walimu wanasimamia na kutekeleza mitaala isiyo rasmi kama michezo na utamaduni ili kuendeleza vipaji vya wanafunzi.
11:Kuhakikisha panakuwepo na kamati za shule zilizo hai na zinazofanya kazi na kuhakikisha kamati hizi zinaendeshwa kwa mujibu wa kanuni, taratibu na sheria.
12:Kumshauri Mkurugenzi kuhusu mambo yote ya Elimu Msingi.
Halmashauri ya Wilaya ya Karatu ina Taasisi za shule zinazomilikiwa na serikali na zisizomilikiwa na serikali kwa shule za msingi ambazo jumla yake ni 107, Idadi ya shule zinazomilikiwa na Taasisi zisizo za kiserikali ni 8, Shule zenye vitengo vya Elimu Maalum ni 3
Halmashauri ya Wilaya Karatu ina jumla ya Walimu 985,pia ina jumla ya wanafunzi 7070 wa shule za awali zinazomilikiwa na serikali na wanafunzi 615 wa shule za taasisi binafsi, wanafunzi wa shule za msingi kuanzia darasa la kwanza hadi la saba kwa shule zinazomilikiwa na serikali ni 47510 na wanafunzi 1721 wa shule za taasisi binafsi. Idadi ya wanafunzi wa MEMKWA ni 421, wanafunzi wa elimu maalum wapo 84
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa