Wanawake vijana na watu wenye ulemavu wametakiwa kuendelea kujitokeza kuomba mikopo ya asilimia kumi kutoka halmashauri ya wilaya ya karatu.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi mtendaji wa halamashauri ya Wilaya ya Karatu Ndg. Juma Hokororo akizungumza katika kipindi cha lango kuu kupitia lumen radio.
Hokororo amesema kwa mwaka 2024/2025 halmshauri ilitoa zaidi ya Bilioni 1.2 kwajili ya mikopo hiyo ambapo kwa wanawake vikundi 97 walipata milioni 725, Vijana vikundi 46 walipata Milioni 486 na wenye ulemavu vikundi 19 walipata milioni 62.
Amesema halmashauri inaendelea kuweka bidii katika ukusanyaji wa mapato yake ili kuendelea kukuza utoaji wa mikopo hiyo ili wananchi wanufaike nayo kama ilivyo tarajiwa na serikali.
Aidha ametoa wito kwa vikundi vilivyokwisha nufaika kuendelea kutumia fedha hizo kwa lengo lililokusudiwa ili kuweza kurejesha kwa wakati nankuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa