Kuandaa mipango kabambe ya afya ambayo inatilia mkazo mahitaji yote ya afya ya halmashauri kwa kuzingatia mwongozo wa Kitaifa wa Wilaya wa mipango ya afya
Kuhakikisha kuwa hospitali, vituo vya afya na zahanati zinatekeleza shughuli za afya, na jamii inamiliki rasilimali kama inavyoelekeza mpango kabambe wa afya wa halmashauri
Kuhakikisha upatikanaji wa usafiri, dawa muhimu, chanjo, madawa, vifaa vya tiba, vifaa na kemikali za maabara katika hospitali, vituo vya afya na zahanati
Kuwa tayari kukabiliana na magonjwa ya milipuko, maafa na kupanga mipango ya kudhibiti na kuzuia
Kuhakikisha kuwa watumishi wa afya walioko katika ngazi mbalimbali kwenye halmashauri wanapata nyenzo za kuwawezesha kufanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa shughuli za afya
Kuhakikisha kuwa huduma za afya zitolewazo zinalingana na viwango vya kitaifa.
Kuhakikisha kuwa halmashauri inazingatia na kufuata sheria zilizowekwa, kanuni, maadili ya kitaalamu na mwenendo wa tabia wa viongozi na watumishi
Kuhakikisha kuwa watumishi wa afya wanakusanya takwimu, wanazichambua, wanazitumia katika mipango, wanatekeleza mipango hiyo na wanatoa mrejesho
Kutambua maeneo ya kipaumbele, kusimamia na kufanya utafiti wa utendaji kazi katika halmashauri
Kujumuisha na kuchambua taarifa za utekelezaji na fedha za robo mwaka na kuziwasilisha kwa Bodi ya Afya ya halmashauri na timu ya uendeshaji wa huduma za afya ya mkoa
Kusimamia mikutano ihusuyo wataalamu wa afya wanaotoa huduma za afya kwenye halmashauri ili kuweza kutambua na kuratibu shughuli zote za afya
Kusimamia na kusaidia huduma za afya ambazo zipo nje na zilizoko mbali kutoka vituo vya kutolea huduma za afya (“outreach services”)
Kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa shughuli za afya kwenye halmashauri
Kumshauri Mkurugenzi Mtendaji kuhusu masuala yote ya afya ndani ya Wilaya