Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Karatu ndugu Juma Hokororo amesema wamefanikiwa kuvuka lengo la ukusanyaji wa mapato katika kipindi Cha miaka miwili mfululizo,huku akisema yote yamewezekana kutokana na elimu ambayo wamekuwa wanatoa Kwa wananchi pamoja na ushirikiano wa timu ya ukusanyaji mapato inayofanya kazi kwa ueledi katika maeneo yote ya Halmashauri.
Amesema bado juhudi za kubuni mbinu mpya za ukusaji wa mapato zinaendelea ambapo ni pamoja na kutoa motisha kwa wakusanyaji mapato na kuanzisha vituo maalumu vya mapato katika kata na tarafa zote.
Ameyasema hayo Leo septemba 24 2025 alipokuwa akihojiwa na Lumen radio kipindi Cha lango kuu,mahojiano zaidi yanapatukana YouTube Lumen Online Tv.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa