Idara ya ujenzi ina wajibu wa kusimamia na kuhakikisha kuwa barabara zote zinapitika kwa mwaka mzima
Idara ina wajibu wa kushirikiana na wadau wengine kubaini, kuandaa, kutathmini na kuchanganua mahitaji ya matengenezo ya barabara mpya na miundombinu mingine kama nadaraja ya chini, makubwa mabawa, na kuziwasilisha kwenye mamlaka za juu kwa hatua zaidi
Idara ina wajibu wa kutayarisha bajeti za mwaka za matengenezo ya barabara katika wilaya kwa mwaka wa fedha mwingine na kuziwasilisha wizarani
Idara ina wajibu wa kuandaa nyaraka za mikataba za matengenezo ya barabar za wilaya
Idara ina wajibu wa kushirikisha kuhusianisha na kuwaunga mkono wadau wengine wafadhili ndani na nje ya wilaya katika masuala ya ushauri wa shughuli za ujenzi, usimamizi na matengenezo
Idara ina wajibu wa kuandaa usanifu wa awali na wa kina wa mabarabara mapya na miundombinu mwingine kwa utekelezaji zaidi katika wilaya
Idara ina wajibu wa kukagua kutathmi ni na kuchanganua kwaajili ya matengenezo mapya na ukarabati wa majengo ya serikali kuwasilisha taarifa kwa mamlaka za juu kwaajili ya utekelezaji zaidi
Idara inahakikisha kuwa majengo na miundombinu nyinginezo za serikali ambazo zimejengwa kwa njia ya mikataba zinakidhi ubora kwa kuonesha uwepo wathamani ya pesa zilizotumika kwa kuwa na usimamizi na utoaji wa kitaalamu ulio makini
Idara ina wajibika wa kutoa huduma za ushauri wa kitaalamu kwa wananchi waliopo wilayani zinazohusiana na ujenzi
Idara ina wajibu kuandaa, kutathmini, kuchanganua na kutunza kumbukumbu za mikataba kwa ajili ya ukaguzi
Idara ina wajibu wa kufanya usanifu kuandaa michoro na miongozo ya bajeti za ujenzi BOQ zitakazohitajika kwaajili ya uzabuni
Idara huwajibika kuandaa bajeti za matengenezo majenzi mapya ya serikali na ukarabati wake kwa mwaka na kuziwasilisha wizarani kwa idhini
Idara ina wajibu wa kuandaa taarifa za mwezi, robo na mwaka za miundombinu ya barabara, majengo na zisizo majengo ya mara kwa mara kwaajili ya kuwasilisha kwenye mabaraza ya kamati ya halmashauri au mamlaka ya juu zaidikwa manufaa ya utawala