Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu Ndg. Juma Hokororo Amewaongoza watumishi wa Halmashauri kutembelea hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro ilio jirani na Wilaya hiyo.
Akizungumza Hokororo amesema kufanya hivyo ni kuunga mkono Juhudi za serikali yq Jamahuri ya Muungano wa Tanzania kuutangaza utalii wa ndani kwa kutembelea vivutio vilivyoko Karibu (TANZANIA THE ROYAL TOUR)
Ameitaja karatu kuwa njiapanda ya utalii nchini Tanzania kwani ni njiaa kuu ya kufika katika hifadhi kubwa tanzania ikiwemo ngorongoro na Serengeti hivyo kwa kutambua hilo halmashauri inazii kuweka bidii ili kunufaika na utalii huo.
Aidha amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Makonda kwa kuendelea kubuni kampeni zinazo tangaza utalii jambo ambalo linawanufaisha wananchi wote mpaka walio na kipato cha chini.
Watumishi hao wa Halmashuri ya Wilaya ya Karatu wamejichanga kwa pamoja kutembelea hifadhi hiyo ya ngorongoro huku wakitaja kuwa ni mwanzo wa kutembelea vivutio vingine zaidi ndani ya tanzania.
Hata hivyo wamemshukuru Mkurugenzi kwa kuandaa na kuhamasisha zoezi hilo kwani limekua na matokeo chanya kwako kama kujenga umoja,Ushirikiano na mawasiliano mazuri baina yao.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa