Maafisa Uandikishaji Wasaidizi na Waendesha vifaa vya Biometriki wa Daftari la kudumu la mpiga Kura awamu ya pili wamekula kiapo leo Mei 14,2025 Mbele ya Afisa Uandikishaji Jimbo la Karatu Eng. Alexander Safari.
Awali kufungua semina ya Uboreshaji wa Daftari la Mpiga Kura awamu ya Pili Ndg. Juma Hokororo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu amewataka maafisa hao kufanyabkqzi kwa weledi na kuishi viapo Vyao.
Aidha amewataka kutunza kwa makinivifaa vinavyotumika katika utekelezaji wa zoezi hilo la uchaguzi na kuepuka uharibifu au upotevu utakao sababisha zoezi hili kutofanikiwa kama ilivyo tarajiwa.
Kufuatia Zoezi la uboreshaji wa Daftari la mpiga Kura awamu ya pili ambalo litaanza Tarehe 16 hadi 22 Mei 2025 Afisa Mwandikishaji Jimbo la karatu Bw. Alexander amewataka Maafisa hao kufanya kazi kwa kufuata taratibu na Kanuni za tume huru ya Taifa ya Uchaguzi na kuepuka awavunji Sheria.
Maafisa Uandikishaji Hao wameapishwa na Mwanasheria Wa Halmashauri Wakili Mussa Makindija ambe kabla ya kuwaapisha ametoa funzo endapo watakwenda kinyume na kiapo hicho.
Uchaguzi wa Mwaka 2025 unaongozwa na Kaulimbiu Isemayo “”JITOKEZE KUSHIRIKI
UCHAGUZI WA MWAKA 2025 KWA AMANI NA UTULIVU”
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa