• Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Complains |
Karatu District Council
Karatu District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dhamira na Dira
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Ujenzi
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
    • Vitengo
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
  • Madiwani
  • Miradi
    • TASAF
    • BOOST
  • Machapisho
    • Hali ya Uwekezaji
      • Business License Form
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Habari
    • Hotuba kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha

RC ARUDISHA TUMAINI KWA WAZEE

Posted on: October 1st, 2020

NA TEGEMEO KASTUS

Wilaya zote zitakuwa na mabaraza ya wazee mpaka kufika mwezi wa kumi na moja mwishoni.Wilaya ambazo mpaka sasa hazina baraza la wazee ni Karatu, Ngorongoro na Longido, baada kuunda mabaraza utaratibu utawekwa kuhakikisha wazee wanashiriki katika vikao vya ngazi zote kuanzia kata mpaka wilaya.

Hayo yamesemwa na Mh. Iddi Kimanta Mkuu wa Mkoa wa Arusha wakati akizungumza katika sherehe ya siku za wazee yaliyofanyika wilaya ya karatu kimkoa, yenye kauli mbiu familia na jamii tuwajibike kuwatunza wazee. Mh. Kimanta ameahidi kuwezesha mkutano wa baraza la wazee la Mkoa amesema mkoa utatoa usafiri kwa viongozi wa Mkoa kutembelea mabaraza ya wazee ya wilaya ili wahamasishe kuunda Mabaraza ya viongozi.

Mkuu wa mkoa wa Arusha Mh. Iddi Kimanta (kulia) akipokea maandamano katika maadhimisho ya siku ya wazee yaliyofanyika katika uwanja wa mazangira bora Karatu

Mh. Kimanta amesema kwa kushirikiana na viongozi wa Mkoa na wilaya katika kusimamia maswala yote yanayohusu wazee, kwa matendo yanayostahili kuwapatia heshima. Ameomba wazee kuwa na imani na serikali, amesema maendeleo yanayofanywa na serikali kila mtu anamchango wake.

Mh. Kimanta amesema mtu yeyote anayebeza wazee hajui anaelekea wapi, Amesema kwa kushirikiana na viongozi  wa mkoa na wilaya huduma za afya kwa wazee zitaimarishwa,  ikiwa na pamoja vitambulisho vya wazee.

Awali katika risala ya wazee iliyosomwa na Mzee Hamisi Ramadhani katibu wa baraza la wazee mkoa wa Arusha amesema dawa za kutibu wazee kwa maradhi yasiyoambukizwa zimekuwa duni na dawa hizo ni gharama kuzipata. Amesema wazee wengi wanaishi katika mazingira magumu inayosababishwa na umaskini na kukosa lishe bora, makazi na huduma nyingine muhimu za  kibinadamu kwa sababu ya hali hii baadhi yao imewasababisha wazee wengine kupata ulemavu ikiwa ni pamoja na miili yao kupooza.

Mzee Ramadhani amesema baadhi ya wilaya kama Meru-dc Arusha-mc, Arusha-dc  zimeanza kuwashirikisha wawakilishi baraza la wazee kwenye vikao muhimu kama vya vikao vya maendeleo vya kata na Wilaya. Mzee Ramadhani ameomba wilaya ambazo haziajatekeleza zianze kufanya hivyo haraka. Amesema  serikali bado haijatunga sheria ya wazee baada ya sera ya wazee iliyotoka takribani  miaka 17, ameomba serikali kukamkamilisha kutunga sheria za wazee  kulingana na mahitaji ya sasa.

Katika taarifa ya Mkoa iliyosomwa na Ndg. Denis Mgiye amesema katika jitihada za kutoa huduma kwa haraka kwenye vituo vya afya wameweka ujumbe unaosema “ kwanza mpishe mzee apate huduma.” Jumla ya mabaraza ya wazee 718 kati ya mabaraza 732 yanayopaswa kuundwa yameundwa katika ngazi ya kijiji mtaa mpaka mkoa. Amesema mkoa umetekeleza maelekezo ya kuwatambua wazee na mpaka sasa wazee  97497 wametambuliwa na wazee wamepatiwa vitambulisho 37262 ambayo ni sawa na 56%.Ndg. Mgiye amesema Halmashauri ya Meru-dc Arush­a-dc Arusha mc na Monduli-dc zinaongoza kwa kuwapatia wazee vitambulisho.

Matangazo

  • Matokeo ya upimaji wa Kitaifa kidoto cha pili January 07, 2024
  • Halmashauri ya Wilaya ya Karatu Uchaguzi wa Wanafunzi wa kidato cha kwanza, 2024 December 18, 2023
  • Matokeo ya Darasa la Nne January 07, 2024
  • KIKAO CHA BARAZA LA MADIWANI 2024 May 11, 2024
  • Angalia Zote

Taarifa Mpya

  • MAAFISA UANDIKISHAJI WALA KIAPO KARATU

    May 14, 2025
  • DED HOKORORO ASHIRIKI KIKAO CHA ALAT WILAYA YA MERU

    May 15, 2025
  • MADAKTARI BINGWA WA SAMIA AWAMU YA TATU WATUA KARAU

    May 12, 2025
  • KARATU WASAPOTIJUHUDI ZA RAIS SAMIA WATANGAZA UTALII WA NDANI

    May 11, 2025
  • Angalia Zote

Video

DC KOLIMBA ATATUA KERO TARAFA YA EYASI KARATU
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fursa za Uwekezaji

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Wizara ya Fedha na Mipango
  • Jamvi la Habari
  • Tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karatu District Council

    Sanduku la Posta: P.O Box 190

    Simu: +255 272970648

    Simu ya Mkononi: 0754773947

    Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa