• Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Complains |
Karatu District Council
Karatu District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dhamira na Dira
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Ujenzi
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
    • Vitengo
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
  • Madiwani
  • Miradi
    • TASAF
    • BOOST
  • Machapisho
    • Hali ya Uwekezaji
      • Business License Form
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Habari
    • Hotuba kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha

ALAT, WARIDHISHWA NA MIRADI YA UJENZI WILAYA YA KARATU

Posted on: December 12th, 2019

Wajumbe wa ALAT mkoa wa arusha wamemaliza kikao chao cha siku mbili wilaya ya karatu.  Baada ya kufanya kikao chao cha ndani amabacho pamoja na mambo mengine wamejadili maadhimio waliyoweka katika Kikao kilichopita.

Mwenyekiti wa ALAT Mhe. Kennedy Sabore Molloimet amekemea kitendo cha wajumbe wa ALAT kutohudhuria vikao hivyo bila taarifa. Mhe. Kennedy amesema kumekuwa na tabia baadhi ya wajumbe kutoa taarifa za udhuru muda wa mwisho kabla ya kuanza kikao jambo ambalo amesema si zuri.

Mhe, kennedy amehimiza Halmashauri kulipa michango kwa wanachama kwa wakati ili kuwezesha utendaji kazi kwa wajumbe wa ALAT. Katika kikao hicho wajumbe wa ALAT walikubaliana kwenda kwenye ziara ya mafunzo mkoani Simiyu

Mhasibu wa ALAT Ndugu Shaban Kisija anasema mfuko wa ALAT ulipaswa kukusanya million 30 lakini mpaka sasa wamekusanya million18,600,000. Bado kuna million 12 inapaswa kulipa kwenye mfuko wa ALAT.

Awali wajumbe wa ALAT walitembelea Miradi minne wilaya ya karatu katika siku yao ya kwanza ya kikao. Miradi iliyotembelewa pamoja na nyumba za walimu mbili two in one na bweni la wasichana Baray Khusumay. Miradi huo ulijengwa na shirika la mafuta duniani   (TPRP-OPEC) awamu ya tatu, kupitia mfuko wa maendeleo ya jamii (TASAF).na uligaharimu  343,824,323.79 kati ya hizo mchango wa wananchi ni shilingi 49.388,299.99 na Tasaf imechangia kiasi cha 294,436,023.80. Mhe. Molloimet Mwenyekiti wa ALAT Arusha na wajumbe  walipongeza nguvu kazi ya wananchi kwa  kufanya ujenzi wa majengo hayo, na walitoa maelekezo kwa watendaji kufikiria namna ya kutengeneza kofia za kuvuna maji ya mvua katika majengo.

WAJUMBE WAKIWA KATIKA MRADI WA NYUMBA SHULE YA BARAY KHUSUMAY

Wajumbe wa ALAT walitembelea pia mradi wa hospital ya wilaya unaojengwa katika kijiji cha Changarawe. Majengo yanayojengwa ni jengo la wagonjwa wa nje (OPD), Jengo la maabara, na jengo la utawala. Ujenzi wa hospital ya wilaya ulianza  baada ya Halmashauri ya wilaya ya Karatu kupokea kiasi cha 500,000,000.00 kutoka mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) kwa ajili ya ujenzi wa miundo mbinu katika hospitali ya wilaya ya Karatu. Halmashauri ilitenga kiasi cha 32,000,000.00 mwaka wa fedha 2018/2019 na kufikisha  jumla ya 532,000,000.00 kwa ajili ya ujenzi wa mradi. Halmashauri imetenga kiasi cha shilingi 40,000,000.00 kwa ajili ya kuendelea na ujenzi.  Mradi huo unatekelezwa kwa njia ya force account. Mhe. Kennedy Mwenyekiti wa ALAT pamoja na wajumbe wa ALAT mkoa wa Arusha wamesema mradi upo katika kasi nzuri, na wametoa maelekezo kwa watendaji wa Halmashauri kufikiria kupanda miti katika eneo la ujenzi wa Hospital.

WAJUMBE WA ALAT WAKIWA KATIKA BOMA LA JENGO LA UTAWALA LA HOSPITAL YA WILAYA YA KARATU

Wajumbe wa ALAT wametembelea ujenzi wa soko kuu la Karatu, soko linalojengwa kwa kutumia fedha za mapato ya ndani. Mradi  ulitarajiwa kutumia shilingi 540,0000,000.00 hata hivyo kutokana na upungufu wa fedha Halmashauri imezigawa hatua za utekelezaji katika awamu mbili.Mwaka wa fedha 2017/2018 jumla ya shilingi 222,000,000,00 zilitengwa kwa phase one ambayo ilikuwa ikihusisha kujenga nguzo na kupaua jengo. Hatua ya pili ilikuwa ni kujenga sakafu; kujenga meza/vizimba, kujenga ukuta, kuweka miundo mbinu ya maji na moto. Utaratibu unatotumika katika ujenzi huu ni kwa kutumia force account. Ujenzi upo katika hatua ya pili na tayari kusawazisha ndani ya soko kumekamilika, ushindiliaji wa eneo la ujenzi umekamilika, usukaji wa nondo kwa ajili ya nguzo na linta (beam) za ghorofa ndogo umekamilika, upangaji wa mawe umekamilika, umwagaji wa zege umefikia 80% na kazi inaendelea na ujenzi wa tofali za msingi upande wa chini wa soko umekamilika. Wajumbe wa ALAT wamepongeza jitihada zilizofanywa katika ujenzi wa soko kuu la mjini Karatu.

WAJUMBE WA ALAT MKOA WA ARUSHA WAKIWA KATIKA MRADI WA UJENZI WA SOKO KUU KARATU

Wajumbe wa ALAT wametembelea ujenzi wa ofisi ya uthibiti ubora wa shule wilaya ya Karatu. Mradi wa Ujenzi wa ofisi za Uthibiti ubora wilaya ya Karatu, umetokana na ufadhili wa fedha za EP4R (lipa kulingana na matokeo) mwaka wa fedha (2018/2019). Wizara ya Elimu Sayansi na technolojia ilitoa  jumla ya Tsh 152,032650. Mradi ulitekelezwa kwa kutumia force account, hadi kukamilika kwa jengo hili kiasi cha 137,032650 kilitumika. 

WAJUMBE WA ALAT MKOA WA ARUSHA WALITEMBELEA OFISI YA WADHIBITI UBORA WA SHULE WILAYA YA KARATU


Matangazo

  • Matokeo ya upimaji wa Kitaifa kidoto cha pili January 07, 2024
  • Halmashauri ya Wilaya ya Karatu Uchaguzi wa Wanafunzi wa kidato cha kwanza, 2024 December 18, 2023
  • Matokeo ya Darasa la Nne January 07, 2024
  • NAFASI ZA KAZI 2024 April 21, 2024
  • Angalia Zote

Taarifa Mpya

  • MILIONI 400 ZATOLEWA KARATU, KUJENGA MABWENI NA MADARASA EYASI SEKONDARI

    January 30, 2025
  • WASIMAMIZI WAASWA KUSIMAMIA VIAPO VYAO KUELEKEA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024.

    November 23, 2024
  • JESHI LA AKIBA MKAWE WAZALENDO KWA TAIFA

    November 23, 2024
  • HALMASHAURI YAZINDUA KITABU CHA MPANGO MKAKATI WA UKUSANYAJI MAPATO.

    November 19, 2024
  • Angalia Zote

Video

DC KOLIMBA ATATUA KERO TARAFA YA EYASI KARATU
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fursa za Uwekezaji

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Wizara ya Fedha na Mipango
  • Jamvi la Habari
  • Tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karatu District Council

    Sanduku la Posta: P.O Box 190

    Simu: +255 272970648

    Simu ya Mkononi: 0754773947

    Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa