Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. CPA Amos Gabriel Makalla amekutana na kuzungumza na Wakuu wa Idara, Maafisa Tarafa, Watendaji wa Kata, Watendaji wa Vijiji na Mitaa pamoja na Wenyeviti wa serikali za Vijiji na Mitaa ya Wilayani Karatu Mkoani Arusha, akiwaagiza kuhamasisha wananchi kushiriki kikamilifu kwenye uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.
Mhe. Makalla katika hotuba yake amesisitiza kuwa kupiga kura ni haki ya Kikatiba kwa kila mwananchi mwenye sifa, akiwahakikishia usalama wa kutosha wananchi wa Wilaya ya Karatu na Mkoa mzima wa Arusha wakati wa kampeni, wakati wa uchaguzi Mkuu na baada ya uchaguzi.
Aidha Mhe. Makalla pia amewasisitiza Viongozi hao kuendelea kutimiza majukumu yao ipasavyo ikiwa ni pamoja na kushughulika na kero za wananchi na kujiepusha kuwa chanzo cha migogoro katika maeneo yao.
“Tuendelee kutatua kero za wananchi, katika hili kuna mahali pengine utawapelekea wananchi kila kitu, wanaona umeme, maji, vituo vya afya na wanakuambia kero yetu moja tu hapa, hatusomewi taarifa za mapato na matumizi kwahiyo Wenyeviti nawakumbusha kusoma ripoti za mapato na matumizi, msiposoma ni kero kwa wananchi na inawarudisha nyuma kwenye hamasa katika kushiriki shughuli za maendeleo.” Amesema Mhe. Makalla.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa