Wilaya ya Karatu ni miongoni mwa Wilaya zilizo nufaika kupitia maadhimisho ya siku ya lishe na Afya ngazi ya kijiji/mtaa.
Hayo yameelezwa na Katibu tawala Wilaya ya karatu Ndg. Bahati Mfungo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Karatu katika maadimisho ya Siku ya lishe na Afya yalio adhimishwa katika Kata ya Mbulumbulu kijiji cha Slahhamo.
Amesema wilaya imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kupunguza matokeo mabaya yatokanayo na ukosefu wa lishe bora kama vile vifo wakati wa kujifungua, kupungua kwa magonjwa yasiyo ya kuambukiza pamoja na udumavu .
Aidha Ndg. Mfungo ametoa rai kwa wananchi kuendelea kuitikia wito wa maadhimisho hayo na kuendea kufata maelekezo ya wataalamu kuhusu afya ya lishe huku akisisitiza kuhusu utoaji wa Elimu kwa Jamii.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu Ndg. Hamza Afisa Elimu Sekondari amesema halmashauri ya Wilaya ya karatu imetenga fedha za kuratibu zoezi la lishe kama ilivyo elekezwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa