NA TEGEMEO KASTUS
Serikali kwa kutambua umuhimu wa wazee ilitengeneza sera maalumu ya wazee ili kuwashirikisha katika shughuli za uzalishaji mali. Ikiwa ni pamoja na kutoa ulinzi wa wazee na kuboresha huduma zinazotolewa kwa ajili ya wazee kama afya kwa kutoa vitambulisho vya wazee ili wapate matibabu bure. Hatua nyingine muhimu zilizofanywa ni pamoja na kuwaelimisha vijana kutambua na kuheshimu maswala yanayohusu wazee katika jamii.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa wilaya ya Karatu Mh. Abbas Kayanda wakati akizindua baraza la wazee wilaya ya Karatu. Mh. Kayanda amesema wazee ni chanzo muhimu cha habari na wanasaidia sana katika kushauri serikali kutokana na uelewa wao mkubwa wa mambo mengi yanayotuzunguka kwenye jamii. Amesema serikali ilianzisha sera ya wazee ya mwaka 2003 ili kuwashirikisha wazee katika mambo yanayowahusu ili kujua hitaji lao ni nini ??. Ameongeza kusema serikali ilianzisha sera ya wazee ili kuwatambua kama rasilimali muhimu katika maendeleo ya taifa.
Mh. Kayanda amesema umuhimu wa baraza la wazee ni kutengeneza jukwaa la wazee ili waweze kukaa na kubadilishana mawazo n kupeana taarifa juu ya mambo ya wazee ya yanavyokwenda katika jamii. Jukwaa hilo linasaidia kuunganisha wazee na kushauri serikali juu ya mambo mbalimbali kwa kujenga mtizamo sahihi kwa jamii. Amesema baraza la wazee linasaidia wazee kukaa kuzungumza changamoto zao zinazowakabili, na kutoa takwimu sahihi ya idadi ya wazee. Amesema kuwa na takwimu sahihi kunasaidia serikali kujua mahitaji sahihi yanayohitajika katika kundi la wazee. Amesema wazee waliopewa nafasi ya kuunda baraza la wazee watasaidia sana serikali katika mambo ya ulinzi na usalama.Mh. Kayanda ametoa rai kwa baraza la wazee kuwa sehemu ya matokeo chanya badala ya kuwa chombo cha kukinzana na serikali.
Mh. Abbas Kayanda (kushoto) akipokea kibao ambacho ataweka kwenye ofisi yake katika ufunguzi wa baraza la wazee wilaya ya Karatu.
Katibu wa baraza la wazee wilaya ya Karatu Daudi Askwari amesema baraza la wazee la wilaya limeundwa na wajumbe wazee saba. Baraza la wazee limeundwa kuanzia January mwaka 2021ili kuwakilisha wazee katika vikao vya maamuzi. Mzee Askwari amesema baraza la wazee litahimiza umoja na mshikamano kwa jamii na mpango wao ni kufanya uzinduzi wa mabaraza ya wazee katika ngazi ya vitongoji, vijiji na kata.
Mzee Askwari amesema ratiba ya uzinduzi itaanzia tarehe 1 -15 mwezi 5 mwaka 2021 mabaraza ya kata ambayo yatakuwa yamezinduliwa. Tarehe 16-17 mwezi june mabaraza ya wazee ya wazee ya vijiji na vitongoji yatakuwa yamezinduliwa. Amesema wawakilishi katika ngazi ya kitongoji vijiji na kata wanatakiwa kushiriki katika vikao vya maamuzi. Amesema wamefarijika kuona wawakilishi wa baraza la wazee la wilaya tayari wameanza kuwakilisha wazee kwenye baraza la madiwani.
Mwenyekiti wa Halmashauri Mh. John Lucian (kushoto) akipokea kibao atakachoweka kwenye ofisi yake.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Karatu Ndg. Waziri Mourice (kushoto) akipokea kibao atakachoweka kwenye ofisi yake
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa