Mbio za mwenge wa Uhuru zimetembelea mradi wa kitalu cha miche ya miti Bashay pamoja na kuzindua klabu ya wapinga rushwa shule ya msingi Bashay. Lengo la mradi huo wa miti ni kuikuza miche ya miti na kuigawa bure kwa wananchi wanaohitaji kupanda miti ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi na uharibifu wa mazingira.
Ndugu Mkongea amesema swala la kupambana na rushwa si la serikali peke yake ni swala la kila mtu. Ndugu Mkongea alizindua kilabu ya rushwa katika shule ya msingi Bashay. Ndugu Mkongeaamepongeza pia jitihada za kijiji cha Bashay kwa kuwa mstari wa mbele katika kutunza mazingira. Ndugu Mkongea ametoa hati ya kuwapongeza wanakijiji kwa jitihada zao za kutunza mazingira.
Awali Mhe. Theresia Mahongo amesema wananchi wa Bashay walipatiwa ardhi muwekezaji wa kampuni ya Mount Kilimanjaro Safari Club. Amesema mazingira rafiki ya uwekezaji ndio yaliyosababisha muwekezaji wa Mount Kilimajaro kuwekeza katika kuhifadhi mazingira.
Ndugu Musa, kushoto akitoa maelekezo ya kitaaalamu ya namna miche ya miti inavyohifadhiwa.
Mradi wa miche ya miti ulianzishwa baada ya ombi la viongozi na wananchi wa kijiji cha Bashay kwa kampuni ya Mount Kilimanjaro Safari Club ili kukabiliana madhara makubwa ya ukame yaliyo anza kuonekana yanayo sababishwa na mabadiliko ya tabia nchi na uharibifu wa mazingira.
Mradi wa HIFADHI MAZINGIRA KIJIJI CHA BASHAY uligharamiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Karatu kwa kutoa wataalam washauri wa misitu na mazingira, Kijiji cha Bashay kikatoa eneo lenye ukubwa wa robo ekari, Wananchi walichangia nguvu kazi ya kuchimba mtaro wa maji wenye urefu wa kilomita 2.3.
Mount Kilimanjaro Safari Club walitoa kiasi cha Dola 33,000 ambazo ni sawa na kiasi cha Tshs 66,000,000/= zilizotumika kama ifuatavyo, Manunuzi ya gari aina ya Toyota Land Cruiser pick up kiasi 37,450,000 ambayo hutumika kusambazia miche ya miti na kupeleka wagonjwa katika huduma ya kitabibu kwa hapa kijijini. Mtandao wa maji toka chanzo cha maji kilomita 2.3 zenye thamani ya shilingi 3,300,000 kujenga uzio wenye thamani 3,000,000 ujenzi wa Jengo la ofisi lenye thamani ya 13,000,000 Samani ya vitu 850,000 Vifaa vya kunyweshea miche yaani keni,mipira n,k vienye thamani 150,000.
Ndugu Musa, kulia akimuelekeza kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa jambo juu utunzaji wa miche ya miti
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa