Na Tegemeo Kastus
Msisitizo watolewa kwa kamati za ujenzi kuongeza uwajibikaji katika miradi ya ujenzi iliyo katika maeneo husika. Lengo likiwa ni kuhakikisha miradi inasimamiwa kuanzia mwanzo wa ujenzi wa msingi na kufuata miongozo ya ujenzi iliyotolewa na serikali. Ujenzi wa miradi hiyo unapokamilika unatakiwa uendane na thamani ya fedha iliyowekwa.
Hayo yamejiri katika ziara ya Mkuu wa wilaya ya Karatu Mh. Abbas Kayanda alipotembelea miradi ya ujenzi inayoendelea katika shule za msingi wilayani Karatu. Katika ziara hiyo Mh. Kayanda ametembelea shule ya msing G-Arusha iliyopewa kiasi cha million 40 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba viwili vya darasa. Ameelekeza kamati ya ujenzi kusimamia vyema ujenzi na kuhakikisha fundi anaongeza nguvu kazi ili ujenzi wa vyumba hivyo vya darasa viweze kukamilika katika muda ulioainishwa kwenye mkataba wa ujenzi.
Mh. Kayanda (kushoto) katika eneo la ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa s/m G-Arusha
Katika ziara hiyo Mh. Kayanda ametembelea shule ya msingi Karatu na kukagua ujenzi wa darasa lilojengwa na mfadhili mpaka hatua ya lenta na kuweka madirisha na milango. Katika ujenzi huo serikali imetoa kiasi cha million 12 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa darasa. Sambamba na kutembelea ujenzi wa chumba hicho cha darasa ameelekeza uongozi wa shule ya msingi Karatu kutoa taarifa ya mchanganuo wa fedha za ujenzi ulivyotumika.
Akiwa katika shule ya msingi Kainam Rhotia Mh. Kayanda ametembelea ujenzi wa madarasa mawili na ofisi yanayojengwa na mdau wa elimu Kamitei foundation. Madarasa hayo mawili yapo katika hatua za umaliziaji na yanatarajiwa kuisha mwishoni mwa mwezi ujao Mh. Kayanda ametembelea ujenzi wa vyumba vingine viwili vya madarasa ambavyo vinafanyiwa ukarabati na wadau wa elimu Kamitei foundation. Amepongeza jitihada hizo za wadau wa elimu zinazofanywa katika shule ya Kainam rhotia ambazo zimelenga kuboresha miundo mbinu ya elimu.
Mh. Kayanda akiwa katika darasa lililomaliziwa kujengwa shule ya msingi Karatu.
Katika hatua nyingine Mh. Kayanda ametembelea shule ya msingi Hareahbi na kujionea ujenzi wa nyumba ya walimu two in one inayojengwa na wadau wa elimu Kamitei foundation. Ujenzi huo umefika katika hatua ya lenta na unatarajiwa kuisha mwishoni mwa mwezi wa kumi. Mh. Kayanda ameonesha kuridhishwa na kasi ya ujenzi wa nyumba hizo. Katika hatua nyingine Mh. Kayanda ametoa kiasi cha mifuko 20 ya saruji kwa ajili ya umaliziaji wa ujenzi wa boma la darasa katika shule ya msingi Hareahbi.
Katika ziara hiyo Mhandisi wa ujenzi, Ndg. Riziki Msite ametoa maelekezo kwa kamati za ujenzi kutoa taarifa kwa mhandisi wa wilaya wa kila hatua ya ujenzi inayofanyika. Ili Mhandisi athibitishe na kujiridhisha na aweze kutoa idhini ya mafundi kuendelea na hatua nyingine za ujenzi. Amesema lengo ni kuhakikisha hakuna makosa yanafanyika ili ujenzi uendane vigezo vilivyotolewa na serikali. Katika ziara hiyo Mhandisi Msite ametoa maelekezo mbalimbali ambayo mafundi ujenzi wanapaswa kuyazingatia ili kutimiza vigezo vya ujenzi katika miradi.
Muonekano wa nyumba ya walimu two in Hareahbi
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa