Wawezeshaji wa mpango na bajeti ya masuala ya lishe kwa ngazi ya mikoa na Halamashauri chini wametoa semina elekekezi kwa wakuu wa idara Halmashauri ya wilaya ya Karatu. Semina hiyo ya siku moja imefanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya karatu.
Mgeni rasmi katika ufunguzi wa Mafunzo hayo Katibu tawala wa wilaya ya Karatu Ndugu Abbas Kayanda amefungua mafunzo ya Bajeti ya Masuala ya Lishe kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya karatu. Ndugu Abbas amesema lazima tupange bajeti ya Mpango wa Lishe na tuweze kuitekeleza bajeti kama ilivyoelekezwa. Amesema kwa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha Halmashauri ya Karatu imetenga million 9,800,000 amemuelekeza mwenyekiti wa kamati ya lishe kuongeza kasi ya utekelezaji wa bajeti ya Mpango wa Lishe.
Ndugu Kayanda amesema ameelekeza wajumbe wa kamati ya lishe kutumia nafasi zao kuwa mabalozi ili kuelimisha jamii. Ametoa maelekezo kwa Afisa Lishe kutembelea vituo vinavyolea watoto kujionea huduma na vyakula wanavyopata. Ndugu Kayanda ameomba viongozi wa dini ambao ni wajumbe kwenye kamati ya lishe kutoa msukumo kwa wazazi na walezi kuhakikisha wanazingatia mpango wa lishe bora kwa watoto wao.
Ndugu abbas Kayanda amesema kuna vikao vinafanyika ngazi ya wilaya ngazi ya tarafa, ngazi ya kata, ngazi ya kijiji, ametoa malekezo kwa Maafisa tarafa, Maafisa watendaji wa kata, na Maafisa watendaji wa kijiji kuzungumzi na kuelimisha jamii kuhusu swala la lishe kama agenda ya kudumu. Ametoa maelekezo kwa (NGOS) taasisi zinazojihusisha na maswala ya watoto kuihusisha na mipango ya serikali ili kuja na mipango yenye manufaa makubwa kwa watoto.
Ndugu abbas kayanda ametoa maelekezo kamati za ulinzi wa watoto kushirikishwa katika Mpango lishe wa wilaya. Amesema wilaya ya Karatu inapaswa kuwa mfano mzuri wa utekelezaji wa mpango na bajeti ya maswala ya lishe ili watu wengine waje wajifunze.
MAAFISA KUTOKA TAMISEMI WAKIMSIKILIZA MGENI RASMI AMBAYE HAYUPO PICHANI
Awali Ndugu Meltoni Nyelaa Mkurugenzi kutoka Tamisemi amesema Wakuu wa Mikoa walishirikishwa katika mkataba wa utekelezaji wa maswala ya lishe na waziri wa nchi tawala za mikoa na serikali za mitaa Mhe. Seleman Jafo. Ndugu Melton ameomba Mkuu wa wilaya na mkurugenzi kusimamia mkataba huu kikamilifu, amesema tathimini ya mpango wa lishe kitaifa itakuwa ikifanywa kila baada ya mwaka mmoja. Amesema TAMISEMI wametoa maelekezo kwa wakuu wa mikoa kufanya tathimini kila nusu mwaka na Halmashauri kila robo ya mwaka. Ndugu Melton amesema matokeo ya tathimini ya mkataba huo yametumika kama chachu ya kuamua aina ya AFUA zitakazoleta matokeo makubwa kwa gharama nafuu. Ndugu Melton amesema kila mwaka wamekuwa wakitenga bajeti ya shilingi 1000 kwa kila mtoto aliyechini ya umri wa miaka mitano kulingana na idadi ya watoto hao katika Halmashauri ili kukidhi matakwa mapambano ya dhidi ya utapiamlo.
WAJUMBE WALISHE WAKIMSIKILIZA MGENI RASMI KATIBU TAWALA WA WILAYA YA KARATU AMBAYE HAYUPO PICHANI
Ndugu Melton amesema maswala ya lishe lazima yawe agenda ya kudumu, swala la lishe liwe sehemu ya mahubiri kwenye sehemu za ibada. Ndugu Melton amesema ni vizuri Maafisa Mipango na makatibu wa afya wawaachie Maafisa Lishe wahusike kikamilifu kwenye mipango ya bajeti ya lishe. Ndugu Melton amesema kwa mwaka huu wa fedha kuna waraka namba mbili wa hazina unaoelekeza namna ya kuingiza shughuli zote za wadau wa maendeleo katika mipango ya bajeti. Amesisitiza hakuna fedha ambazo zitakuwa zinatumika ambazo ziko nje ya bajaeti, ndugu Melton amesema kuanzia sasa Maafisa lishe watakuwa wajumbe wa HRMT, CHMT ili wajikite katika kupanga AFUA za bajeti ya Mipango ya Lishe katika ngazi hizo.
Mwenyekiti wa lishe wilaya Ndugu Waziri Mourice amesema amepokea maelekezo ya Mkurugenzi kutoka Tamisemi juu ya bajeti ya Mpango wa lishe. Amemuelekeza Afisa mipango wa Halmashauri kuhakikisha hapunguzi bajeti ya Mpango wa Lishe. Ndugu Waziri Mourice amesema tukipunguza bajeti kwenye Lishe tunasababisha afya ya watoto wetu kuathirirka na utapiamlo, amesema mwaka ujao wa fedha lazima tupange bajeti ya kujitosheleza kwenye lishe. Ndugu Mourice amesema mwaka ujao wa fedha Halmashauri itapanga bajeti marambili, ya bajeti halisi ili kuweza kufikia malengo ya bajeti ya Mipango Lishe.
WAJUMBE WA LISHE WILAYA YA KARATU KATIKA PICHA YA PAMOJA NA MGENI RASMI KATIBU TAWALA WA WILAYA YA KARATU (ALIYEPO KATIKATI) KATIKA WAJUMBE WALIOKAA
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa