NA TEGEMEO KASTUS
Barabara ya Lositete Mpaka Selela ambayo ilifanyiwa ukarabati na wananchi kipindi cha nyuma inahitaji gharama kubwa kukamilika utengenezwaji wake. Taarifa hiyo ya ukarabati wa babaraba hiyo ilitolewa kwenye kikao cha ushauri cha barabara cha mkoa.
Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya ya Karatu Mh. Theresia Mahongo katika kikao cha mwisho cha baraza la madiwani. Mh. Mahongo amesema barabara zinazounganisha wilaya moja na nyingine ni barabara ambazo zipo chini ya Tanroad na sio Tarura. Amesema kutokana na upembuzi yakinifu barabara ya Lositete Selela uliofanywa na Tanroad, amesema Tanroad wamepokea taarifa ya ukarabati wa barabara Lositete ambayo inatokea wilaya ya Monduli na wamesema fedha zitakaporuhusu wataiweka kwenye bajeti yao na wataifanyia kazi. Amesema kwa upande wa Karatu barabara hiyo ilishafunguliwa na imebaki wa upande wa pili wa wilaya nyingine.
Sambamba na hilo Mh.Mahongo amesema kuna ujenzi mpya wa kipande cha barabara ya lami km 1, amesema tayari wakala wa barabara vijijini Tarura walikuwa wanatafuta mkandarasi wa kujenga kipande hicho cha barabara ambacho kitajengwa maeneo ya katikati ya mji karibu na soko jipya.
Watendaji wakiwa katika kikao cha baraza la madiwani
Mwenyekiti wa Halmashauri Mh.Emmanuel Gege amesema swala la Muwekezaji kukarabati eneo la barabara ya Makoromba kwenda makao makuu ya wilaya waliridhiana kwenye kikao rasmi na muhtasari wa kikao upo. Amesema kwa sababu walikaa na muwekezaji huyo pamoja na mambo mengine waliyokubalina ilikuwa ni kurudisha eneo la wananchi kiasi cha ekari 100 kwa wananchi. Mh.Gege amesema muwekezaji akumbushe juu ya utekelezaji wa ahadi zake kabla hatua zaidi hazijachukuliwa.
Awali Mh, Benedicto Modaha amesema wanachi wa Makoromba wanapata adha ya usafiri kutokana na barabara hiyo ya kuja Makao makuu ya wilaya kuhitaji ukarabati mkubwa. Amesema kuna mwekezaji aliahidi muda mrefu kujenga barabara hiyo lakini bado barabara hiyo haijatengenezwa mpaka sasa.
Diwani wa Endamarariek Mh. John Lucian amesema utengenezaji wabarabara ile ya Lositete uligharimu takribani million 100 na wananchi walijitolea kusaidia ujenzi wa barabara ile kutokana na adhaa ya usafiri kipindi cha nyuma ambayo iliwalazimu wananchi kuitengeneza. Amesema awali kulikuwa na changamoto za kukatika kwa barabara kipindi cha masika katika eneo la kirurumo baada ya daraja kujaa maji.
Amesema barabara ya Lositete mpaka Selela ilikuwa ni barabara mbadala, ameongeza kusema mtu wa Lositete akitaka kwenda selela ni km 5 lakini sasa wananchi wanazunguka njia ya Manyara Mto wa mbu kigongoni kwenda selela mzunguko unaokadiriwa kufika km 30. Ameomba waandisi kuja na mpango wa ambao utasaidia utekekelezaji wa kuijenga barabara hiyo.
Injinia safari Deemay kwa niaba ya meneja wa Tarura Amesema wamepeleka mapendekezo kukarabati barabara za Karatu zilizoharibika kutokana na mvua kali zilizonyesha kipindi cha mvua. Amesema kunauwezekano Karatu mjini km 9m mpaka 10 za barabara zilizoharibika zikachongwa na kuwekwa vizuri zaidi na zoezi hilo linatarajiwa kufanyika mwezi wa sita mwishoni au mwezi wa saba mwaka huu.
Injinia Deemay amesema wanatengeneza barabara vipande vipande kwa sababu ya uwezo wa fedha mdogo ukilinganisha na mahitaji makubwa yanayohitajika. Hivyo huanza kwa kuangalia maeneo korofi kwanza kabla ya kushughulika na maeneo mengine. Ili barabara iweze kupitika kipindi chote cha mwaka bila matatizo.
Amesema swala la barabara ya Makoromba kuelekea Makao makuu ya wilaya muwekezaji aliahidi kujenga barabara kwa umbali wa km 9 na sehemu iliyobakia ilikuwa imaliziwe na wakala wa barabara wa vijijini. Muwekezaji huyo alitaka kuweka alama za mipaka ya ardhi katika eneo lake la uwekezaji wakati akiendelea na zoezi hilo la ukarabati wa kipande cha barabara alichoahidi kukitengeneza lakini mvutano wa muwekezaji na wananchi juu ya zoezi hilo ulisababisha kila kitu kusimama ikiwa ni pamoja na ujenzi wa barabara hiyo.
Mkazi wa karatu ndg. Mathias Lazaro amesema mvua za masika zimefanya uharibifu mkubwa wa barabara. Amesema barabara zinaharibu sana vyombo vya usafiri amesema mathalani sehemu korofi ambazo wateja wa boda wanahitaji kupelekwaa na kuchukuliwaa huku wakihitaji bei taafifu . Amesema barabara zikifanyiwa ukarabati zitasaidia kurahisha huduma ya usafiri kwa maana ya gharama, lakini pia itawapunguzi adha ya kukarabati vyombo vya usafiri mara kwa mara.
waheshimiwa madiwani wakiwa katika kikao cha baraza
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa