Na Tegemeo Kastus
Wananchi wanaotegemea usafiri wa umma kutoka na kuingia kata ya Mbulumbulu watakiwa kuvaa barakoa ili kuzuia kusambaa na kujikinga na virusi vya corona. Azimio hilo limeafikiwa na wajumbe wa kikao cha maendeleo ya kata wakati wakiajadili janga la virusi vya corona.
Kikao hicho cha maendeleo ya kata kimefanyika katika makao makuu ya kata ya Mbulumbulu, pamoja na hatua hizo kikao kimeazimia kufunga sehemu zinazouza pombe za kienyeji, sehemu zinazohusika na uchezaji wa Pooltable na Karata kwa kipindi hiki cha janga la corona. Kikao hicho pia kimejadili desturi ya watu kulala wengi kwenye kirago kimoja na kuazimia kujikita katika kuelimisha jamii kuchukua tahadhari katika sehemu za kulala kwa kuacha tabia ya watu kulala wengi katika kirago kimoja.
Mhe. Elias Simpa amesema bado wananchi hawajahamasika kunawa mikono mara kwa mara amesema ni vyema tukahamasisha wananchi wapate muamko wa kunawa kwa maji yanayotiririka na sabauni. Mhe. Simpa amesema kuhamasisha kila familia iwe na sehemu ya kunawa mikono kwa maji tiririka na sabauni sambamba na hilo ametoa rai kwa wananchi juu ya shughuli za misiba. Amesema ili kupunguza uwezekano wa kupata maambukizi, Halmashauri imetoa maelekezo angalau wingi wa watu kwenye msiba usizidi watu 30.
Mhe. Simpa ametoa hofu wajumbe juu ya maendeleo ya ujenzi wa barabara amesema katika ujenzi wa barabara bado mkandarasi yupo eneo la kazi na amesimama kutokana na mvua kubwa zinazoendelea. Amesema anaendelea kufanya mawasiliano na wadau mabalimbali ili kuunganisha nguvu katika kutenengeneza barabara katika maeneo ambayo mkandarasi hatafika hasa barabara za makao makuu ya kata pamoja na barabara ya Lositete mpaka makao makuu ya kata.
Mwenyekiti wa kikao cha maendeleo ya kata ya Mbulumbulu Mhe.Elias Simpa akisisitiza jambo
Naye Mtendaji kata wa Mbulumbulu Ndg Elikana Sulumbu amesema eneo la kilimamoja limekuwa maarufu kwa utengenezaji wapombe haramu gongo. Amesema vita ya kongo ni vita ya muda mrefu, walishawahi kukamata lita zaidi ya 300 kijiji cha Slahhamo na kumwaga pombe hiyo kwenye mkutano mkuu wa kijiji. Lakini bado juhudi hizo zimekuwa zikipata upinzani mkubwa kutoka kwa watengenezaji hao wa pombe. Amesema pombe ya gongo inadhoofisha afya ya mwili, amesema hizi pombe za kienyeji za kawaida zinachanganywa na gongo ili kuongeza kilevi zaidi.
Pombe hiyo imekuwa ikisafirishwa kwa njia za uchochoro na kuibeba kwa vifungashio tofauti tofauti ili kujenga mazingira ya usiri katika usafirishaji. Ndg. Sulumbu amesema wenyeviti wa vitongoji wanapaswa kuanza kudhibiti kwenye maeneo yao ili isisambae kwenye maeneo mengine. Kuna orodha ya watu sugu ambao wameshakamatwa mara kwa mara kwa kujihusisha na matukio ya gongo, kikao hicho cha maendeleo ya kata kimeazimia kuanza na orodha hiyo kwa umakini mkubwa wa kutengeneza ushahidi na kuwapeleka mahakani badala ya kutegemea jeshi la polisi.
Wajumbe wa kikao wamebaini namna jeshi la polisi, linavyowarudisha nyuma katika vita ya kukabiliana na gongo. Wajumbe wamesema Lositete kunamitambo midogo midogo ambayo inatengeneza gongo kali ile inayosisimua ubongo haraka. Biashara hiyo ya gongo imekuwa kama mtaji kwa jeshi la polisi, ambao hukamata watuhumiwa wa gongo na kuwachia bila hatua za kisheria kuchukuliwa zaidi. Kikao hicho kimeazimia kushirikisha jamii ili iweze kulaani matumizi ya pombe hiyo ya kienyeji, wakati hatua zaidi zikiendelea kuchukuliwa na viongozi katika ngazi mbalimbali.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa