• Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Complains |
Karatu District Council
Karatu District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dhamira na Dira
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Ujenzi
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
    • Vitengo
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
  • Madiwani
  • Miradi
    • TASAF
    • BOOST
  • Machapisho
    • Hali ya Uwekezaji
      • Business License Form
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Habari
    • Hotuba kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha

UMUHIMU WA TECHNOLOJIA NA ATHARI ZAKE KWA MAZINGIRA

Posted on: February 11th, 2020

Teknolojia ni nyenzo nyepesi inayomsaidia binadamu kutumia vyombo ili kurahisisha kazi.Technolojia ni neno ambalo limetoholewa kutoka neno la kiingereza technology.  Asili ya neno technology ni lugha ya kigiriki "τέχνη" (tamka: tékhne):  lenye maaana ya „uwezo, usanii, ufundi".Technology ni elimu inayohusu uhandisi, ufundi, ujenzi, vifaa na mbinu za uzalishaji wa vifaa na huduma katika jamii kwa mujibu wa Wikipedia.

Teknolojia inaweza kumaanisha: vifaa na mashine zinazotumika katika matengenezo au uzalishaji wa vitu elimu ya matumizi yake pamoja na mbinu na maarifa jinsi ya kutumia sayansi uwezo wa kubadili malighafi asilia na kuwa bidhaa yenye thamani inayoweza kukidhi mahitaji ya binadamu. Hapa bidhaa haimaanishi tu vitu kama magodoro, magari ya kutembelea, unga wa ngano n.k., la hasha: ni huduma yoyote inayotolewa kwa jamii, mfano huduma ya usafiri, huduma ya utalii, huduma ya chakula, na pamoja na vitu vyote vinavyozalishwa viwandani.

Taarifa mojawapo ya cnn iliyochapishwa katika tovouti tarehe 29/1/2020 imeelezea ugunduzi wa techonolojia mpya, juu ya wadudu ambao wametengenezwa kwa vinasaba vya kibailojia kukabiliana wadudu wa mwituni wanaoharibu mazao na wanao hatarisha afya ya binadamu ugunduzi umefanyika kwa mafanikio makubwa. Wadudu hao bandia (feki) waliotengenezwa kibailojia kwa vinasaba na  kufanana kabisa kwa umbo la almasi kwa nyuma (diamond back moth) waliachiwa kwa mara ya kwanza huko New York kubabiliana na wadudu halisi ambao ni waharibifu wenye umbo lao halisi la almasi kwa nyuma (diamodd back moth).

Utafiti huo unaonesha ni rahisi kutumia viwavi bandia waliotengenzwa kwenye maabara kisayansi kwa kutumia vinasaba vya viwavi halisi; kuzuia viwavi hao waharibifu, kuleta madhara na hasara kwa mazao. Hiyo inatokana tafiti za nyuma kuonesha viwavi halisi ambao wanaharibu mimea kuwa imara na kukabiliana viwatilifu vinavyotumiwa kuwaua. Hivyo wataalamu kuamua kutengeneza viwavi bandia kukabiliana na viwavi halisi ambao wamekuwa wakileta hasara kubwa kwa mazao.

Utafiti wa kutumia viwavi bandia kuangamiza viwavi halisi uliandaliwa na Oxitec Developer of insect biological control. Ambao wanafahamika kwa kutengeneza mbu bandia waliokabiliana kupunguza mbu kubeba homa ya Dengue  na  Malaria. Utafiti Oxitec hivi sasa umejikita katika kutengeneza maisha ya muda mfupi ya mbu bandia anapoangua mayai. Hata hivyo  utafiti wao hivi sasa umejikita katika kutengeneza viwavi bandia kwa kukusudia kupunguza ongezeko lao kwa kutumia (antibiotic) tetracycline kuua viwavi wa kike pindi wanapotumia chakula chao bandia wanapotaka kuongeza idadi bandia ya viwavi wa kiume ili waweze kuendelea kuazaliana bila kuleta madhara.

Utafiti huo ulienda mbali kwa kutengeneza mbu wa bandia kwa vinasaba vya mbu halisi, chapisho la cnn kwenye tovouti yao tarehe 18 /Jul /2019. Umeonesha mafanikio makubwa katika visiwa vya Guandong china uliondoa mbu wenye asili (Asian tiger Mosquito) ambao kwa 94%  walichangia kuleta maambukizi ya maradhi. Hali hiyo ilichangia kushuka kuumwa na mbu  kwa watu kwa kiwango kikubwa hadi kufikia 97% ya watu kutoumwa na mbu. Professor matafiti Xi Zhyoung katika chuo cha Michigan state amekuwa mmoja mwa watu waliojikita sana katika utafiti wa kutumia mbu dume aliyezuiwa kisayansi kuzalisha (sterilized) kujamiana na mbu wa kike ambaye hajazuliwa (unaltered) ili kujararibu kupunguza kuzaliana kwa wingi kwa mbu.

Utafiti ukaenda mbali kwa kuzuia uwezo wa mbu wa kike kuendelea kuzaa (sterilized) na  mbu wa kiume waliamua kutumia mfumo wa (wolbachia bacteria) ambao ni mfumo wa kibailojia wa kugawa bacteria wenye madhara wasiendelee kuleta madhara kwa viumbe hai wengine. Utafiti huu ulifanyika kipindi kinacho aminika ni cha uzalianaji mkubwa wa mbu 2016-2017 katika visiwa viwili huko Guangzhou city.

Matokeo ya zoezi hilo ni kukaribia kuondoa mbu wa kike katika visiwa hivyo na tamko lilotolewa na mtaalamu wa Ekolojia Peter Armbuster anasema lilikuwa ni jaribio liloangamiza na kuua mazingira magumu ya kuishi. Licha ya kwamba mbu aina (Asian Tiger Mosquito) ilikuwa ni ngumu kuwaondoa lakini ilibidi watumie madawa, na kuharibu mayai  makazi  sehemu zenye maji.

Mbu wenye michirizi mieupe (White stripped Mosquito) inasemekana ni mbu walioleta madhara makubwa huko Asian na wamesambaa mabara mengi kulingana na utafiti. Shirika la afya duaniani limesema Mbu wanasababisha hatare kubwa ya kifo kwa binadamu kutokana na kuzaliana sana. Lakini pia kusambaza magonjwa hatare kama homa ya Dengue na Malaria.

 Afisa Mazingira wa wilaya ya Karatu Ndugu Ally Mdangaya  anasema kila utafiti unaofanyika lazima uwe na muendelezo wa utafiti mwingine mpya. Lazima utafiti mwingine wa kina ufanyike juu ya ugunduzi wa kutumia wadudu bandia wenye vinasaba vya mdudu halisia. Hata kama wadudu hao watakuwa wanatabia za mdudu halisi kuna vitu au sifa watakuwa wanakosa kutoka kwenye mdudu halisi wa kawaida. Hivyo kuleta changamoto nyingine mpya kwenye mazingira ambayo nayo yatahitaji kufanyiwa utafiti mwingine wa kina ili kuitatua.

Ndugu Mdangaya anasema mfumo wa ekolojia wa viumbe hai wanyama na mimea na binadamu unategemeana. Wanyama kwa namna moja au nyingine wanategemea mimea kwa chakula lakini pia kwa kujihifadhi. Wadudu wanategemea mimea kwa chakula na kujihifadhi hali kadhalika kwa binadamu. Mimea inategemea ndege na wadudu kwa ajili ya uchavushaji wa mimea. Kuharibu mfumo huu wa kutegemeana kwa viumbe hai ni kuleta changamoto nyingine kubwa zaidi. Mathalani kunguru weusi wa Zanzibar waliletwa kutoka India ili kusadia kuua wadudu  wanaosababisha ugojwa wa minazi lakini baadae wakageuka kuwa kero kwa sababu wadudu waliisha na baadae kungururu wakaleta uchafuzi mkubwa wa mazingira.

Ndugu Mdangaya anasema wadudu bandia waliotengenezwa wataleta tattizo kwenye mfumo wa Ikolojia. Kutatua changamoto moja kisayansi kunaleta changamoto nyingine ya kisanyansi, anasema kipindi cha nyuma Mtwara kulikuwa na shida ya panya wanaofanya uharibifu mkubwa wa mazao. Wakaletwa nyoka wenye uwezo wa kula panya lakini baadae nyoka walipoisha ikawa tatizo kubwa kwa binadamu.

Ndugu Mdangaya anasema viwavi ni viumbe waliopo kwenye mfumo wa ikolojia, hatupaswi kuegemea kwenye kutumia dawa.  Ili kutunza mazingira kama eneo linalima Mahindi na viwavi wanashambulia Mahindi basi mkulima inabidi abadili zao la kilimo ili viwavi wasije kuathirika. Hiyo ndio namna inayopendekezwa katika jitihada za kutunza mazingira ili kukabiliana na viwavi waharibifu.

Matangazo

  • Matokeo ya upimaji wa Kitaifa kidoto cha pili January 07, 2024
  • Halmashauri ya Wilaya ya Karatu Uchaguzi wa Wanafunzi wa kidato cha kwanza, 2024 December 18, 2023
  • Matokeo ya Darasa la Nne January 07, 2024
  • NAFASI ZA KAZI 2024 April 21, 2024
  • Angalia Zote

Taarifa Mpya

  • MILIONI 400 ZATOLEWA KARATU, KUJENGA MABWENI NA MADARASA EYASI SEKONDARI

    January 30, 2025
  • WASIMAMIZI WAASWA KUSIMAMIA VIAPO VYAO KUELEKEA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024.

    November 23, 2024
  • JESHI LA AKIBA MKAWE WAZALENDO KWA TAIFA

    November 23, 2024
  • HALMASHAURI YAZINDUA KITABU CHA MPANGO MKAKATI WA UKUSANYAJI MAPATO.

    November 19, 2024
  • Angalia Zote

Video

DC KOLIMBA ATATUA KERO TARAFA YA EYASI KARATU
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fursa za Uwekezaji

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Wizara ya Fedha na Mipango
  • Jamvi la Habari
  • Tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karatu District Council

    Sanduku la Posta: P.O Box 190

    Simu: +255 272970648

    Simu ya Mkononi: 0754773947

    Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa