NA TEGEMEO KASTUS
Mkuu wa wilaya ya Karatu Mh. Theresia Mahongo amekemea vitendo vya utovu wa nidhamu vinavyofanywa na wanafunzi. kuna wanafunzi wamevunja madarasa, wamevunja vifaa vya walimu na kutaka kupiga walimu na matokeo yake serikali imechukua hatua kwa watoto waliojihusisha na fujo hizo kutofanya mtihani wa kumaliza kidato cha sita.
Mh. Mahongo ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa semina ya kupinga ndoa za utotoni Karatu iliyoandaliwa na wadau wa elimu shirika la world vision. Semina iliyohusisha tarafa za Endabash na Eyasi ikijumuisha watendaji kata, waratibu wa elimu kata na watu wa afya. Mh. Mahongo amesema Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Karatu Ndg. Waziri Mourice alienda kuzungumza na wanafunzi lakini alivyoondoka wanafunzi wakaenda kukoleza moto. Mh. Mahongo amesema wanafunzi hao wa Karatu sekondari walitaka kuchoma gari, amesema wamejihusisha na kung’oa nyaya za umeme na kuiba computa.
Mh. Mahongo amesema wazazi jana wamekuja wanaona kwamba watoto wao wameonewa. Amesema niliuliza wazazi hao kama watoto 365 waliotajana na kutambuana wahusika wa fujo hizo na kupatikana wanafunzi 21 nani atakuwa amemuonea ?? Mh. Mahongo amesema wanafunzi hao walikamatwa kama wahalifu kwa sababu ni vijana wakubwa na bodi ya shule ilifanya maamuzi yake kulingana na utaratibu wa serikali. Amesema wanafunzi hao watalipa kulingana na uhalifu waliofanya. Mh. Mahongo amesema chanzo cha fujo hizo ni simu ya mkononi.
watendaji wakifuatilia kwa makini semina ya kupinga mimba na ndoa za utotoni wilayani Karatu.
Mh. Mahongo ameomba wazazi na viongozi wa dini kusaidia katika kulea watoto wawe na tabia njema. Amesema taifa lenye maadili ni taifa linaloweza kujiendesha. Mh. Mahongo amesema kuna wakati walikamata watoto wa shule sekondari Welwel wakiwa wanajiuza miili yao.
Mh. Mahongo amesema unajiuliza wazazi wao wanawaaangalia hawa mabinti ?? anasema ukimufuatilia mtoto kwa mzazi unakuta mzazi hana habari. Amesema kuna baadhi ya familia baba na mama ni walevi hivyo watoto wanajilea wao wenyewe.
Mh. Mahongo ametoa wito kwa wazazi kuwajibika katika malezi ya watoto wao, amesema ipo siku sisi tutaulizwa mbele ya mwenyezi Mungu tumefanya nini ?? na hatutakuwa na majibu kwa sababu hatujatumia nafasi zetu vizuri. Mh. Mahongo amesema walimu huwa wanatoa taarifa kwa wazazi juu ya mienendo ya watoto wetu, wazazi tunafanya ufutiliaji gani kwa watoto.
Mh. Mahongo amesema mwaka huu kuna kesi 14 za watoto wa sekondari waliopata mimba na kesi mbili kwa wanafunzi wa shule ya msingi. Mh. Mahongo amesema hii ni hasara kubwa kwa taifa, Mh. Rais Dkt. John Pombe Magufuli anatoa fedha nyingi kuwezesha wanafunzi kupata elimu. Lakini pia ni hasara kubwa kwa mzazi pindi mtoto anapopoteza fursa ya kupata elimu.
Mh. Mahongo amesema kumekuwa na mazoea wazazi kupeana madume, kondoo pindi mwanafunzi wa kike anapopata mimba kwa kisingizio watoto wameungana damu, ametoa maelekezo kwa watendaji kata kuwakamata wazazi wa pande zote watakao jihusisha na matendo hayo.
Dkt. Elipendo Ombay (kulia) wakati akiwasilisha taarifa
Amesema mtu anayewapa mimba wanafunzi anaweza kufanya kitendo kama hicho kwa mwanafunzi mwingine. Amesema wazazi wanatabia ya kuwakingia vifua watoto wao hata kama wamefanya makosa. Hatupendi kabisa kushirikisha katika malezi jambo linalochangia kuongezeka kwa watoto wasio na madili.
Mratibu wa world vision Ndg. Merian Leyla amesema wanawezesha wananchi katika miradi ya ufugaji mbuzi wa maziwa, ambao yanasaidia familia katika kuimarisha kipato cha familia. Miradi hiyo inasaidia wazazi kuwa na uwezo wa kupata mahitaji ya mtoto wa kike. Amesema katika kusaidia kumlinda mtoto wa kike kwa kuanzia shirika la world vision limejenga bweni katika shule ya msingi Gidamilanda kusaidia wanafunzi wa kike. Amesema tayari wameshapata watoto 70 watakao kaa bwenini wanaotoka katika jamii hiyo wafugaji.
Ndg. Leyla amesema kuna miradi ya maji ambayo pia shirika la world vision inashughulikia kama shule ya sekondari Baray. Amesema miradi ya maji imejengwa ili kuwapa kipaombele watoto wa kike wasiende umbali mrefu kupata maji na kuingia katika vishawishi vya ngono.
Amesema kuna kilimo cha Mbogamboga ambacho pia kinamsaidia mzazi uwezo kupata mahitaji ya shuleni pamoja na mahitaji mengine. Amesema kazi kama hizo zinampa Mzazi muda mwingi wa kukaa nyumbani na kumlea vizuri mtoto. Amesema sambamba na hilo kuna semina mbalimbali za walimu na wazazi zinazofanywa ili kuwajengea uwezo wa namna ya kumlinda mtoto wa kike.
Matukio mbalimbali wakati wa uwasilishaji wa mada
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa