NA TEGEMEO KASTUS
Kilele cha Maadhimisho ya siku wa wakulima kimefanyika katika viwanja vya nanenane Njiro mkoa wa Arusha maadhimisho hayo yataendelea kwa siku mbili zaidi kabla ya kuhitimishwa. Banda la Halmashauri ya wilaya ya Karatu ni miongoni mwa wilaya zilizoshiriki katika maonesho hayo Mjini Arusha.
Madhimisho hayo nane nane yenye kauli mbiu Kwa maendeleo ya kilimo mifugo na uvuvi chagua viongozi bora 2020 yameleta hamasa kubwa kwa wananchi waliohudhuria na kujionea vitu mbalimbali vilivyokuwa sehemu ya maonyesho. Pamoja na banda la kilimo kulikuwa na banda la mifugo la Halmashauri ya wilaya ya karatu. Tunaleta habari kwa njia ya picha kwa baadhi ya matukio yaliyotokea katika kilele cha maadhimisho ya nanenane.
AFISA KILIMO NDG. WAYDA AKIONESHA NAMNA KAHAWA ILIYOKAANGWA INAYVOWEZA KUSAGWA NA MASHINE NA KUPATA KAHAWA YA UNGA.
AFISA UVUVI ELISANTE FRANK (KUSHOTO) AKIELEZEA UFUGAJI WA SAMAKI KATIKA BWAWA MAALUM LA SAMAKI KWENYE BANDA LETU LILOKUWA NA SAMAKI AINA YA KAMABALE.
WANANCHI WAKISIKILIZA MTAALAMU WA KILIMO (KULIA) AKIELEZEA KILIMO CHA NYANYA KATIKA BUSTANI YETU ILIYO KATIKA BANDA LA HALMASHAURI YA KARATU.
MBUZI AINA YA SAANEN KATIKA BANDA LA MIFUGO WANAOPATIKANA KATIKA SHIRIKA LA FOOD FOR HIS CHILDREN NI MBUZI WANAOWEZA KUZAA MARA MBILI KWA MWAKA NA KIVUTIO KIKUBWA KATIKA MAONESHO YA NANENANE.
KATIKA BANDA LA MIFUGO KUNA WATOTO WA SUNGURA WA KISASA AINA YA CALFORNIA WHITE AMBAO WANAOHIMILI KUISHI MAZINGIRA YOTE. SUNGURA HAO WAKIKUA WANAWEZA KUZAA WATOTO 7-11 NA WANAUZITO WA KG 3.5- 4.5. LAKINI PIA KUNA KUKU WA KISASA SASSO AMBAO WANAKUWA KWA HARAKA NA WANASTAHIMILI MAGONJWA WANAFIKA KILO 1.8-2.5 KWA MUDA WA MIEZI MINNE.
BANDA LA MIFUGO LINA NG'OMBE WA KISASA MWENYE UWEZO WA KUKAMULIWA LITA 30 KWA SIKU KWA MAANA YA KUKAMULIWA LITA 15 ASUBUHI NA LITA 15 JIONI NI MOJA YA KIVUTIO KATIKA BANDA LETU LA NANENANE.
PICHA YA JUU WANANCHI WAKIANGALIA KILIMO CHA MBOGAMBOGA CHA KWENYE MIFUKO MBELE YA BANDA LA KILIMO LA HALMASHAURI YA KARATU NA CHINI NI MWANACHI AKIULIZA MAHITAJI KWENYE MEZA YA KUUZA VITUNGUU NDANI KATIKA BANDA LA HALMASHAURI YA KARATU.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa