Afisa elimu sekondari ameanza ziara ya kutembelea shule zote za sekondari wilayani Karatu. Ziara hiyo imejikita katika kuangalia na kukagua mikakati ishirini na tano aliyowaelekeza walimu wa sekondari kama inatekelezwa. Lakini pia kuangalia jitihada na ufanisi wa walimu katika kuinua kiwango cha kitaaluma.
Katika ziara hiyo ambayo amefanya Tarafa ya Eyasi ameambatana na watendaji wa wilaya wa idara ya elimu sekondari wa ngazi ya wilaya. Bi, Kalista Maina akiwa sekondari ya Qangdend amebaini udhaifu mkubwa wa kiufundishaji kwa walimu wa shule hiyo. Bi, Maina amesema walimu hao hawajishughulishi na kuandaa andalio la somo darasani lakini pia kuna udhaifu mkubwa wa ujazaji wa (class journal) daftari la kusaini walimu wanapofundisha au kuingia darasani.
Afisa elimu Bi, Maina amesema walimu wa shule hiyo hawafuatilii maelekezo aliyoyatoa ya kuzingatia mikakati ya ishirini na tano aliyotoa. Bi, Maina amesema faili la akiba ya maswali ya mitihani ya kitaifa hawana ya kujitosheleza, hawafuatili notice wanazowapa wanafunzi. Mahudhurio ya kusuasua kwa walimu, na kuzembea kujaza kitabu cha kujaza mahudhurio ni moja ya dosari za wazi wazi zilizoonekana. Katika ziara hiyo walimu wawili hakukukutwa katika kituo cha kazi, na ruhusa zao za kutokuwepo kazini zimeweka mashaka.
Afisa elimu sekondari kulia, Bi Maina katika ukaguzi
Bi. Maina amesema shule ya Qangdend imekuwa ya 32 na ya Mwisho kwa matokeo ya mtihani wa Moko na imekuwa shule ya 224 kati ya 226 za mkoa wa Arusha. Bi, Maina amesema walimu wa shule hiyo hawajali ufundishaji na matokeo yake watoto wamekuwa na ufaulu duni. Bi, Maina amesema shule hiyo ina walimu watatu ambao watoto wamepata â Fâ darasa zima katika mtihani wa Moko kidato cha nne. Walimu hao ni mwalimu wa historia, hesabu, na biology.
Bilogy kwa muhula uliopita wa masomo, kuna vipindi 52 kwa kidato cha kwanza, na vipindi 34 havijafundishwa kwa kidato cha pili na kidato cha tatu vipindi 14 jumla kufika vipindi 100. Vipindi vya historia kidato cha kwanza 33 na vipindi vya kidato cha pili 14 kidato cha tatu kidato 11 na kidato cha nne 10 kufika jumla ya vipindi 68 ambavyo havijafundishwa. Vipindi vya hesabu ambavyo havijafundishwa kwa kidato cha pili ni 24 na kidato cha tatu ni vipindi 8 na kidato cha nne 10 hivyo kufanya vipindi kufika 42 kwa muhula uliopita.
Bi, Maina amesema kwa hali jinsi ilivyo taarifa ataipelekea kwa Mkurugenzi, ambaye ni mwajiri wa watumishi. Ili aweze kuchukua hatua stahiki za kinidhamu, ameongeza kusema kutokufundiha na kuanda andalio la somo ni kosa ambalo linaweza kukusababisha kufukuzwa kazi. Bi. Maina amesema hatuwezi kulaumu watoto tu wakati ufundishaji wa walimu unasuasua.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa