Mkoa wa Arusha una kiwango kidogo cha maambukizi ya malaria kwa kuwa na kiwango cha chini ya 1% kulinganisha na mikoa mingine ya Tanzania bara. Hayo yalisemwa na Dkt Fabrizio Molten Mtaalamu mshauri kitengo cha malaria, katika kikao cha Wadau wa afya kilichofanyika Karatu siku ya Jumatano.
Dkt. Fabrizio alisema uambukizo kitaifa ni 7% na uambukizo wa ndani kwa Arusha umetoweka kuna wastani wa wagonjwa wa malaria 1.5 kwa watu 1000. Mkoa wa Arusha inapata mgonjwa 1 kwa mwezi kwa kila Kituo cha Afya. Halmashauri ya Longido Ngorongoro kiwango cha maambukizi ni kidogo zaidi ambayo 0.5 % na Halmashauri ya Karatu, Monduli na Meru ni kidogo zaidi. Arusha dc, Mjini na Jiji Uambukizo ni Mkubwa kwa sababu wanapata wageni wengi.
Dkt. Fabrizo alisema mikoa yote 26 ya Tanzania Bara Arusha ni mkoa wa mwisho kwa kuwa na maambukizi ya malaria, hiyo inaonesha kwamba arusha ni mkoa wa kwanza kwa kutokuwa na maambukizo ya Malaria kali katika wilaya zake zote, ukilinganisha na mkoa wa Kigoma uanongoza.Mambo yaliyochangia kuondoka kwa Malaria ni pamoja na maendeleo ya kijamii, katika ujenzi wa nyumba bora, hali ya hewa bora kuwa na nyuzi joto 16, ambayo imechangia vimelea haviwezi kutimiza mzunguko wake ndani ya mbu. Hatua zilizo chukuliwa awali na serikali zimechangia, Arusha ilikuwa awali katika kiwango cha 15% ya mambukizi ya Malaria miaka10 iliyopita ukilinganisha na sasa.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa