Sherehe za siku ya mtoto zimefanyika katika uwanja wa shule ya msingi Endabash. Sherehe hizo zimejumuisha watoto kutoka sehemu mbalimbali katika wilaya ya karatu.Ujumbe wa mkoa kutoka ustawi wa jamii ulitoa taarifa ya matukio ya unyanyasaji wa watoto kwa mkoa wa Arusha.
Ndugu Simoni Panga kamishina wa ustawi wa jamii mkoa amesema, watoto wanapata athari za unyanyasaji wa kihisia, ndoa za utotoni na mimba za utotoni. Amesema mkoa wa Arusha ulikuwa na watoto 54911 wanaoishi mazingira hatarishi na watoto 19421 kati yao wameunganishwa na huduma mbalimbali kama, afya na elimu ambayo ni sawa na 35%. Bado kuna 65% hawajapata huduma hii ni kwa mujibu wa takwimu za March mwaka huu kutoka kitengo cha ustawi wa jamii mkoa.
Ndugu Simoni amesema kuna mahakama 13 zinazosikiliza mashauri ya watoto mkoa wa Arusha. Mashauri ya watoto 193 yamefikishwa mahakamani kuanzia julay 2018 mpaka march 2019. Jumla ya watu 1437 kwa mwaka (2017-2018) walifanyiwa ukatili wa kijinsia katika mkoa wa Arusha na wahanga wakubwa walikuwa wanawake na watoto, hii ni kwa wale ambao taarifa zao zilifika vituo vya afya na polisi. Ndugu Simoni amesema wameanzisha kituo cha kutoa huduma kwa wahanga wa kijinsia (one stop centre) kitengo hicho kimeanza kuanzia mwezi wa tano mwaka huu hospitali ya Mount Meru Arusha. Ndugu Simoni amesema wahanga wa kijinsia hawahitaji kupata rufaa ili kupata matibabu kwenye kituo hicho.
Ndugu Simoni amesema wamefanikiwa kuwa na kamati ya ulinzi wa mwanamke na mtoto kwa ngazi ya mkoa na kila wilaya. Kamati 506 zimeundwa kati ya kamati 687 sawa na 74%. Ustawi wajamii mkoa wamefuatilia mashauri ya watoto wanaokinzana na sheria kupitia mahakama za watoto zilizoteuliwa na kuna mashauri ya watoto193 tangu ( Jualai 2018-march 2019 ).
Nalo shirika la world vision limetoa semina katika mabaraza ya watoto katika vijiji 32 vya Tarafa ya Endabash na Eyasi. Ndugu Danile Kirhima amesema wametoa mafunzo ya haki za watoto, na takribani watoto elfu moja walifikiwa katika mafunzo hayo. Mafunzo kwa kamati ya ulinzi wa mtoto na pia yamehusisha viongozi wa dini takribani themanini na viongozi wa jamii na serikali miamoja. Shirika la world vision limetoa elimu pia kwa taasisi zote za elimu, wazazi walimu vijana na wanafunzi. Ndugu Daniel amesema shirika linatoa ushirikiano kwa serikali kuhakikisha watoto wanalindwa na wanaendelezwa ili waweze kufikia malengo yao.
Ndugu Daniel mratibu wa world vision ametoa raia kwa wazazi, amesema mzazi ndiye mdau wa kwanza anayeweza kuandaa msingi wa mtoto. Ameomba wazazi kufuatilia mienendo ya watoto wanapokuwa shuleni.
Watoto wakifuatilia jambo wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa