Na Tegemeo Kastus
Naibu waziri wa kilimo Mheshimiwa Omary Mgumba amefanya ziara katika Halmashauri ya Karatu jana. Ziara hiyo ya Naibu Waziri ililenga kujionea shughuli za kilimo na umwagiliaji, na amefanya mkutano kijiji cha Jobaj katika Tarafa ya Eyasi na kusikiliza kero za wananchi.
Mh. Mgumba amesema Halmashauri ya Wilaya ya Karatu inakusanya billion tatu ya mapato. Katika mapato hayo kilimo cha vitunguu kinachangia 29% ya mapato. Mh. Mgumba ameelekeza wananchi kujenga visima kuvuna maji ya mvua ili yasipotee bure, amewaelekeza wananchi kujiunga na vyama vya ushirika kila kijiji ili waweze kukopesheka na taasisi za kifedha ili waweze kununua zana za kisasa za kilimo.
Mh. Mgumba amesema 20% ya mapato ya Halmashauri yapelekwe kwenye sekta ya kilimo ili iweze kuwasaidi wakulima. Fedha hizo zitumike kama mitaji kwa wakulima, hayo ni maelekezo ya serikali kwa Halmashauri zote. Mhe. Mgumba amesema anafahamu kuna mvutano wa maji ya umwagiliaji kati ya magereza na wananchi. Mh. Mgumba amesema magereza nao wanahitaji maji kwa shughuli zao na kwa ajili kilimo cha umwagiliaji, amesema kuna miradi nane ya maji na mradi mmoja unatumiwa na magereza.
Mh. Mgumba amesema kuna mradi wa utengenezaji wa bwawa la maji la magereza wa miaka 10 iliyopita. Mradi huo umeshindwa kutekelezeka, Mh. Mgumba amesema serikali kupitia wadau wa maendeleo Japan imetoa zaidi ya shilingi 300 millioni lakini bado bwawa halifanyi kazi. Mh. Mgumba amemuelekeza Mkuu wa Wilaya kuunda tume kuchunguza mradi huo.
Mh. Mgumba ametembelea chanzo cha maji na amewaelekeza wananchi kuhifadhi vyanzo vya maji. Amesema kuacha chanzo cha maji wazi kinakauka, Mh. Mgumba ameelekeza wananchi na serikali kupitia Halmashauri waandae miche ya miti na magereza wao wataipanda. Mhe Mgumba amesema ni vizuri wakapanda miti ya matunda ambayo ni rafiki wa maji katika chanzo ili waweze kukilinda chanzo hicho cha maji. Mh. Mgumba amewaelekeza wananchi wanaojishughulisha na kazi za uzalishaji ndani ya mita 60 za chanzo cha maji au mito wanatakiwa kuondoka kwenye vyanzo hivyo vya maji.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa