Serikali imetangaza kutotumia mifuko au vifungashio vya plastic nchi nzima kuanzia tarehe mosi mwezi wa sita. Halmashauri ya wilaya ya Karatu ilishapiga marufuku matumizi ya vifungashio vya plastic kabla na kuweka azimio la kuzuia mifuko ya plastic pamoja na kupitisha sheria kwenye baraza la madiwani.
Kaimu Afisa mazingira na usafirishaji wa wilaya ya Karatu Ndugu Jacob Gadiye ameishukuru serikali kwa hatua hiyo. Idara ya mazingira itasimamia na kutekeleza agizo la serikali la kutotumia vifungashio vya plastiki, isipokuwa vifungashio vya plastiki vyenye bidhaa kutoka viwandani. Ametoa wito kwa wananchi kuheshimu na kutekeleza agizo la serikali. Ndugu Gadiye amesema vifungashio vya plastiki vina madhara makubwa sana kwa afya ya binadamu, mazingira na wanayama.
Ndugu,Gadiye amesema vifungashio vya plastiki vimetengenezwa kwa kemikali na rangi ambayo ikipata joto inayeyuka. Watu wanatabia ya kubeba vyakula vya moto kwa vifungashio vya plastiki hivyo kuyeyusha rangi pamoja na kemikali na kuingia kwenye chakula, ambayo ni hatari kwa afya ya binadamu. Kemikali ile inapochanganyikana na chakula, mtu anapokula kile chakula kemikali inaingia mwilini, kwenye mfumo wa damu, ini na figo. Hivyo baadae kusababisha matatizo kama saratani; watu wanapata matatizo ya figo, na matatizo ya ini.
Ndugu Gadiye anasema vifungashio vya plastiki vinamadhara hata kwa mifugo, asilimia kubwa ya mifugo inayochinjwa ndani inakuta imemeza vifungashio vya plastiki. Mifugo inatabia ya kupenda kula vitu vyenye ladha ya chumvi chumvi inapokula vifungashio vya plastiki inakuwa ngumu kupata mmeng’enyo. Joto la tumboni inasababisha kifungashio cha plastiki kilichopo ndani kuanza kuyeyuka na kutoa rangi ambayo inaingia kwenye damu ya mnyama. Hivyo mnyama anapochinjwa mlaji anakula ile kemikali iliyoingia kwenye mfumo wa damu wa mnyama aliyechinjwa lakini pia husababisha mnyama pia kufa kutokana na kukwama kwenye tumbo la mnyama.
Ndugu Gadiye anasema kwa upande wa mazingira, mifuko inatapakaa maeneo mengi na inasabaisha uchafu wa mazingira. Mfuko ili uoze unachukua miaka mia tano lakini pia unapochoma mfuko ile harufu yake ni mbaya kwa afya ya binadamu. Inaleta adhari ya upumuaji kwa afya ya binadamu kwa afya mimea pia inaleta athari kwa mfumo uchujaji wa mionzi ya jua angani. Hivyo kusababisha dunia kupata mvua mbaya za asidi, lakini pia kuongeza joto kubwa kwenye dunia
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa