Kikao cha baraza la madiwani kimekaa leo ili kupitisha bajeti ya maendeleo ya serikali mwaka 2019/20. Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya karatu na kilikuwa na ajenda moja tuu ya kujadili bajeti.
Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Jublate Mnyenye ndiye aliyeongoza kikao. Mwenyekiti alianza kwa kusoma barua ya mabadiliko ya asilimia ya mapato ya ndani kwa Halmashauri ambayo inapaswa kutumika katika miradi ya maendeleo na ile inayopaswa kutumika katika matumizi ya kawaida. Barua hiyo yenye kumbu. Na.CE.CCE.325 / 387 / 02 / 13 ya tarehe 12 / Feb / 2019 kutoka Tamisemi, imesema madaraja yanaendelea kuwa mawili ( A na B ) kama ilivyo sasa. Daraja A lina Halmashauri 16 na daraja B lina Halmashauri 169, Halmashauri zilizo katika daraja A zitatumia 40% ya mapato yake ya ndani kwenye matumizi ya kawaida, na 60% itatumika katika miradi ya maendeleo. Halmashauri za daraja B zitatumia 40 % ya mapato katika miradi ya maendeleo na 60% ya mapato kwenye matumizi ya kawaida.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Ndugu, Godfrey Luguma amesema bajeti lazima iboreshwe na iendane na kilichoelekezwa kulingana na barua ya mabadiliko ya bajeti waliyoipokea kutokea Tamisemi.
Mhe. John Lucian amesema jambo hilo ni kubwa na wakitaka wakae vikao vyote na walipwe wataadhiri bajeti iliyopo mbele. Ameomba busara kutumika, kwani kutoka 60% kwenda 40 % fedha zitakazo toka ni kidogo, amewaomba waheshimiwa madiwani kujitoa kwenye jambo hilo kwa sababu hali ni mbaya kwenye vyanzo vya ndani vya mapato ya Halmashauri.
Mhe. William Qambalo amesema kwa namna bajeti iltakavyoainishwa itafanya madiwani watafute fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi katika maeneo yao. Amesema ni vyema swala la bajeti likapitia tena katika kamati ili kuweza kujua miradi ambayo itafanyiwa kazi katika mwaka ujao wa fedha.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa