Kikao cha baraza la madiwani kimejigeuza na kukaa kama kamati kujadili changamoto za jamii ya wahadzabe bonde la Eyasi. Baada ya baraza hilo kumaliza kupokea taarifa za kamati za kudumu za Halmashauri za robo ya kwanza ya mwaka.
Mhe. Theresia Mahongo Mkuu wa wilaya ya Karatu ametoa maelekezo kwa baraza la madiwani kuchukulia uzito swala la jamii ya Wahadzabe, baada ya wawakilishi wa wahadzabe kutoa taarifa maalum ya changamoto zianazowakabili. Mhe Theresia amesema baraza litoe maelekezo na lije na majibu ya ufumbuzi wa changamoto zinazowakabili jamii ya wahadzabe.
Madiwani wakifuatilia kikao katika ukumbi wa Halmashauri
Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe.Emmanuel Gege amesema baada ya baraza kujigeuza kamati, wameweka maazimio kuenda maeneo husika ili waweze kuainisha changamoto ili waziunganishe changamoto mpya na zaawali. Amesema wametengeneza utaratibu baada ya baraza kujigeuza na kukaa kama kamati wameazimia viongozi wa maeneo husika kulinda wa maeneo wanayoishi jamii ya Wahadzabe. Amesema malengo ni kubadilisha mfumo uliopo wa sasa wa wahadzabe na kuboresha maisha yao. Amesema changamoto kubwa ni kwamba jamii ya nyingine zinavamia na kufanya shughuli za kibinadamu katika maeneo ya wahadzabe licha ya ukweli kwamba maeneo hayo yamepimwa na kutengwa kwa ajili ya matumizi ya wahadzabe.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Karatu ndugu Waziri Mourice amesema jamii ya wahadzabe ni kivutio cha watali kwenda kutembelea jamii ya wahadzabe kujifunza namna wanavyoishi. Amesema waongoza watalii wanawalaghai wageni kwamba jamii ya wahadzabe hawajui kiswahili na hawajui fedha. Amesema kuwaita wawakilishi wa wahadzabe kwenye baraza ni ili kusikiliza changamoto wanazopata na kuzipatia ufumbuzi.
Ndugu Waziri Mourice amesema mazingira ya maisha waliyokuwa wanaishi zamani yamebadilika, kuna shule ya Msingi Endamaghan ambayo ni shule ya bweni na ambayo ilianzishwa ili kuisaida jamii ya wahadzabe na Hayati Mwl Julius Kambarage Nyerere rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ndugu Waziri amesema jukumu la kusaidia jamii ya wahadzabe na kutetea maslahi yao ni la serikali. Amesema jamii ya wahadzabe maisha waliyokuwa wanaishi zamani na sasa hivi ni tofauti, amesema ni kweli walikuwa wanategemea uwindaji lakini hivi sasa jamii nyingine zimeingia na kufannya shughuli za kibinadamu katika maeneo wanayoishi hivyo kuondoa mazingira ya uwindaji kama zamani. Hivyo kufanya jamii hiyo kuanza kuishi kwa kutegemea nafaka kama chakula.
Awali katika taarifa yao iliyosomwa na Bi Mariam Anyawile amesema wamekuwa wanaishi bonde la Eyasi kwa muda mrefu na baadae jamii nyingine kuanza kuja katika bonde hilo kutafuta makazi na kufanya shughuli za kibinadamu. Ameongeza kusema jamii ya Kihadzabe imekuwa ikipewa kiasi kidogo cha fedha kwa watalii wanaoenda Tarafa ya Eyasi. Bi, Mariam amesema katika mchakato wa uboreshaji wa utalii unaoendelea Eyasi bado kuna mambo mengi hawayafahamu. Amesema sintofahamu hiyo inawasababisha kujiuliza maswali kama mkachakato huo kama utatoa ufumbuzi wa matatizo yao.
Watendaji wakiwa katika kikao cha baraza la madiwani
Bi. Mariam amesema biashara ya utalii imekuwa haiwapi mafanikio ya moja kwa moja katika maisha yao. Kumekuwa na wageni kutoka nje ya nchi ambao wanataka kufahamu uhalisia wa maisha yao ya porini, na ukarimu wao kwa watalii ni ili kufanya wageni waondoke na kumbukumbu nzuri.
Naye Padre Miguel Angle wa Mang’ola anayeishi na kusadia jamii ya wahadzabe Tarafa ya Eyasi, amesema hela iliyopatikaba kwa jamii mwezi wa kumi katika geti la utalii Eyasi ni shilingi 3469000 kwa mwezi. Amesema mathalani matumizi ya wahadzabe kwa mwezi wa kumi, anasema mahitaji ya kuwapeleka hospital jamii kwa mwezi wa kumi ni shilingi 500040. Wametumia million 2500,000 kwa wagonjwa, Kafteria ya chakula kwa wagonjwa wanaolazwa 820,000. Siku ya shabaha ambayo wanafanya kila tarehe 4 shilingi 250,000, chakula walichogawa kwa jamii shilingi 250,132. Gharama za kuwaleta Karatu kwenye tamasha la utalii shilingi 340,000, kiliniki tunayofanya nao mara mbili kwa mwezi shilingi 500,000. Matumizi kwa ujumla wake kwa mwezi shilingi 7500,000 mapato ya getini shilingi 3500,000, Padre Miguel amelieleza baraza mahitaji ameyabeba kwa muda wa mrefu, lakini sasa anaweza kuondoka, je akiondoka nani atawasaidia watu wa jamii ya khadzabe wanaoishi bonde la Eyas.
Padre Miguel amesema kwa miaka 8 mfululizo kila mwezi wamekuwa wakiwalisha kwa chakula gunia 15-20 za mahindi na maharage gunia 3, mafuta kilo 55 na hii yote inahitaji fedha. Padre Miguel amesema utalii ndio tegemeo lao la maisha kwa sasa baada ya wanyama kupotea mizizi kuwa shida kupatikana kwa sababu ya watu kuanzisha shughuli zao za mashamba. Pato lao la utaalii kwa mwezi haliendani na mahitaji ya jamii ya wahadzabe kwa mwezi. Padre Miguel anasema bei yao ya kupokea utalii, tangu ilivyopangwa mwaka 2008 mpaka leo haijapanda. Jamii nyingine tozo ya fedha zao kwa ajili ya utalii zinapanda, anasema kwanini isiwe wao ?? Padre anasema wahadzabe wanafanya kazi siku nzima na watalii wanalipwa 20000 kwa jamii nzima, tofauti na tozo ya jamii nyingine zinazowazunguka zinazofanya kazi za utalii masaa machache tofauti na wahadzabe. Padre Miguel amesema anashutumiwa anafanya biashara ya utalii na jamii ya wahadzabe, amesema lakini madai hayo siyo kweli.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa