Bodi ya huduma za afya ya wilaya ya Karatu imezinduliwa jana na Mkuu wa Wilaya ya Karatu Mhe. Theresia Mahongo katika Ukumbi wa Halmashauri ya Karatu. Mhe. Theresia amewaomba wajumbe walioteuliwa kusaidia kuboresha sekta ya afya.
Mhe. Theresia Mahongo amesema tangu tumepata uhuru maadui wetu wamekuwa ni elimu maradhi na tatizo la uchumi; serikali imeendelea kutatua mambo ya elimu kwa kutoa elimu bure, kujenga madarasa na kutoa mikopo kwa wanafunzi masikini katika ngazi ya elimu ya juu. Katika sekta ya afya serikali imeongeza bajeti na ameomba wajumbe wazipitie bajeti vizuri. Ameomba watendaji kutoa ushirikiano kwa bodi ili kufanikisha malengo ya serikali, Mhe. Theresia amesema hatapenda kuona migongano kati ya (watumishi) sekretarieti na bodi.
Dkt. Mustafa Waziri Mganga mkuu wa wilaya amesema katika taarifa yake hali ya utoaji huduma imeboreka, Wilaya Karatu mwezi 12 wakinamama waliojifungua kituo cha afya Karatu ni 188 ambayo ni zaidi ya mara tatu ya awali.
Dkt. Mustafa amesema ICHF mfuko wa afya ulioboreshwa usajili unafanyika kwa kutoa Tsh 30000 kwa watu sita. Utaratibu wa uwanaandikishaji ni kwenye zahanati na picha ya mtu aliyeandikishwa itakuwepo kwenye kituo ulichojiandikisha, hospitali ya wilaya, na hospitali ya mkoa. Mwananchi aliyelipia ICHF iliyoboreshwa kwa watu sita inamwezesha yeye na wanufaika wa mfuko kutibiwa na kupata rufaa ya matibabu hospitali ya wilaya na hospitali ya mkoa.
Dkt, Mustafa amesema upatikanaji wa dawa muhimu kwenye vituo afya ni kwa asilimia 97.9, amesema wana akiba ya chupa za damu 1272 ambayo ni sawa na asilimia 85, na kwa kanda ya kaskazini Wilaya ya Karatu ni ya kwanza kwa kuchangia damu. Karatu inawastani wa kutumia chupa tisini hadi mia moja kwa mwezi. Kupitia mpango wa Big result now (BRN) wamepandisha vituo vya afya vienye nyota tatu kumi na mbili na tumepunguza vituo vienye nyota sifuri kumi na mbili mpaka kufikia vituo vitatu.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa