Na Tegemeo Kastus
Serikali iko mbioni kufanya marekebesho katika muundo wa bodi ya maji ili kuongeza ufanisi na uwajibikaji wenye tija kwa wananchi. Dhamira ikiwa ni kuongeza uwazi na ushirikishwaji wananchi katika maswala yanayohusu utoaji wa huduma ya maji.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa wilaya ya Karatu Mh. Abbas Kayanda alipokuwa akizungumza katika mkutano wa hadhara na wananchi wa Kainam Rhotia. Mh. Kayanda ameitaka bodi ya maji Mowasu kutafakari juu ya kiwango cha bei ya shilingi 210,000 iliyokuwa ikitozwa ili kusaidia kujenga mtandao wa maji. Amesema gharama hiyo sio rafiki kwa wananchi kwa sababu licha ya gharama hiyo mwananchi anatoa fedha zaidi, kama gharama ya kupata huduma ya maji kwa kugharamia kununua mita ya maji, kugharamia kuchimba mtaro kwa ajili ya kutandaza mabomba ya maji.
wananchi wakiwa katika mkutano wa hadhara katika kijiji cha Kainam Rhotia
Mh. Kayanda ameitaka Ruwasa kuangali viwango vya bei ya unit moja ya maji inavyotozwa na Mowasu. Amesema Mowasu wanapopanga bei ya viwango vya maji wanapaswa kuwashirikisha wananchi katika mikutano ya Halmashauri ya kijiji. Ameelekeza bodi hiyo ya maji Mowasu kuhakikisha taarifa za mapato na matumizi ya bodi yao inasoma kwenye Mikutano mikuu ya Halmashuri ya kijiji ili wananchi waweze kupata uelewa wa pamoja juu ya namna bodi ya maji inavyojiendesha.
Mh. Kayanda amesema serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais. Mh. Samia Suluhu Hassan imetoa kiasi cha million 320 kwa ajili ya kurekebisha na kutengeneza miundo mbinu ya maji katika kata ya Rhotia. Amesema fedha hizo zinalenga kuondoa adhaa ya maji ambayo wananchi wanapata kutokana na miundo mbinu ya maji kujengwa kwa muda mrefu. Amesema licha ya ujenzi ya miundo mbinu ya maji serikali kupitia wakala wa barabara Tarura itachonga barabara kuanzia Rhotia mpaka shule ya msingi Juhudi katika jitihada za kuimarisha miundo mbinu ya usafiri Kainam Rhotia.
Matukio mbalimbali wananchi wakiwa katika wa mkutano
Katika hatua nyingine Mh. Kayanda amezungumzia kuhusu umeme wa Rea three round one uliokuwa unafanywa na Mkandarasi NIPO ambaye amesitishiwa mkataba. Amesema mkandarasi wa sasa ni kampuni tanzu ya Tanesco na tayari mafundi wako eneo la mradi mpaka mwezi wa kumi mwaka huu nguzo zilizokuwa zimesimama nyaya zitawekwa na wananchi watapata huduma ya umeme.
Mh. Kayanda ametemebela mradi wa zahanati ya kijiji cha kilimatembo ambao uko katika hatua za mwisho za ujenzi wake. Ameridhishwa na kasi ya ujenzi ambao unaendelea huku matarajio ya kukamilisha ujenzi wa choo na maliwato na ukitarajiwa kuishwa mwsihoni mwa mwezi wa tisa. Mh. Kayanda ameelekeza wakala wa maji vijijini kufanya upembuzi yakinifu ili kuwezesha huduma ya maji kufika katika zahanati ya kilimatembo.
Mh. Kayanda akiwa katika zahanati ya kilimatembo
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa