Mkuu wa Wilaya ya Karatu Mhe. Theresia Mahongo leo amefanya mkutano wa hadhara na wananchi wa Kambi ya Simba. Katika mkutano huo Mhe. Theresia Mahongo amewaomba wananchi wa kijiji cha Kambi ya Simba kuendelea kutunza amani.
Katika mkutano huo Mhe. Theresia Mahongo alipata nafasi ya kusikiliza pande zinazovutana juu ya sehemu ya ardhi ambayo Chama cha Ushirika Kambi ya Simba kinailalamikia Halmashauri serikali ya kijiji cha Kambi ya Simba kwa kutwaa ardhi yao.
Mhe. Theresia Mahongo amesema ndani ya muda wa wiki mbili mvutano wa Chama cha Ushirika Kambi ya Simba na serikali ya kijiji cha Kambi ya Simba juu ya uhalali wa eneo linalomilikiwa Chama Cha Ushirika utapatiwa ufumbuzi. Mhe. Theresia amesema busara itatumika kutatua mvutano huo, amesema chama cha ushirka ni chetu na kijiji pia ni chetu.
Mhe. Theresia amesema serikali inataka kuimarisha Vyama Vya Ushirika, amehimiza wananchi kujiunga kwenye Chama Cha Ushirika. Amesema ushirika sio wa watu wachache, jambo la msingi ni kufuata taratibu za kujiunga na Chama Cha Ushirika, ameomba wananchi kutoa taarifa kama kuna mtu anawakataza watu wasiingie kwenye Chama Cha Ushirika. Mhe. Theresia ameshangazwa na chama cha Ushirika kuwa na wanaushirika arobaini tuu na ameahidi kulifuatilia kwa undani kwanini watu hawajiungi na Chama Cha Ushirika.
Mhe. Theresia amewahimiza wananchi kuwapeleka watoto shule, amesema kamata kamata kwa wazazi ambao watashindwa kupeleka watoto shule itaanza. Amewaomba wananchi kuwapatia watoto chakula wanapokuwa shuleni. Mhe. Theresia amesikitishwa na ufaulu duni wa wanafunzi katika mtihani wa kidato cha nne. Mhe. Theresia amewahimiza wazazi kuwaendeleza masomo ya ufundi watoto ambao hawakufanya vizuri katika mitihani yao ya mwisho katika chuo cha Veta.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa