Masomo ya computa kwa vituo vinavyoendeshwa na Compassion International kwa kushirikiana na Elim pentekoste Karatu yamefunguliwa leo kwenye kituo cha watoto cha compassion kilichopo karibu na eneo la Tanesco Karatu.
Ndugu Lameck Karanga amesema jambo hilo ni zuri, nchi zilizoendelea zimefika mbali kwa kuwekeza kwa kutumia technolojia ya computa. Amesema serikali watatoa ushirikiano kwa mambo wanayofanya na ameomba jitihada hizo za kuwaendeleza watoto hao kwa mafunzo ya computa ziende mpaka kwenye shughuli za serikali zilizopo karibu. Pamoja na mafunzo hayo pia kituo hicho kimeweka program ya vitabu ambavyo vitawasaidia vijana hao kujisomea.
Mkurugenzi wa kituo cha T.A.G Ndugu Amani Lohay amesema wanashukuru serikali kwa kutambua mchango wao. Amesema mafunzo hayo yatajumuisha wanafunzi 32, kutoka katika vituo vinne ambavyo ni Elim pentekoste ambacho kimetoa wanafunzi 10, Karatu mjini 7, ELCT Oldean 8, na T.AG Bashay 7. Mafunzo hayo ya awali kwa sasa yatadumu kwa muda wa wiki moja.
Ndugu Lohay amesema mafunzo hayo yamelenga kuwajengea wanafunzi tabia ya kusoma vitabu kwa kutumia program maalum inayohifadhi vitabu kwenye computa. Amesema wamedhamiria kuwapanua vijana maarifa kwa kuwaelekeza na kuwafunza program mbalimbali zitakazowasaidia katika maendeleo yao siku za baadae. Mafunzo hayo pia yamelenga kuwajenga wanafunzi kiroho.
Wanafunzi wakisikiliza kwa makini katika mafunzo ya kutumia computa
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa