Na Tegemeo Kastus
Taasisi ya Community aid and social education empowerment (CSEE) kwa kushirikiana na Child fund Korea ambao wamejikita katika kusaidia watoto dhidi ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona wametoa msaada wa vifaa vienye thamani ya million 40 kwa wilaya ya Karatu.
Msaada huo ni vifaa vya kukabiliana na virusi vya corona pamoja na spika za sauti za kusaidia kuelimishia jamii sehemu mbalimbali zenye shughuli zinazokusanya watu wengi pamoja. Mkuu wa wilaya ya Karatu Mh. Theresia Mahongo ameshukuru taasisi ya CSEE kwa msaada waliotowa kwa wananchi wa Karatu. Amesema taasisi hiyo imegusa vijana wetu wengi hasa kwa kipindi hiki ambacho vyuo na shule za sekondari za kidato cha tano na sita zikiwa zimefunguliwa. Amesema msaada umekuja wakati sahihi na kamati ya wilaya ya covid-19 itakaa kikao ili kuweka mpangilio mzuri wa ugawaji wa vifaa kwa watoto katika shule.
Mh. Mahongo amesema bado anaendelea kutoa elimu kwa watu mbalimbali juu ya namna ya kujikinga na virusi vya corona. Ameomba taasisi hiyo kujikita katika kambi za wavuvi tarafa ya Eyasi pamoja na sehemu za minada. Amesema muda mzuri wa kutoa elimu kwenye kambi ni jioni saa kumi ambao ni muda watu wengi wanakuwa wanarudi kwenye mialo . Mh. Mahongo amepongeza juhudi zilizochukuliwa na Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania katika kukabiliana na covid-19.
Afisa wa mradi wa CSEE Ndg. Ombeni Sakafu amesema taasisi inafanya kazi na watoto amesema vifaa hivyo vitasambazwa katika shule. Amesema wametoa barokoa 500 N95 lakini Gun themometre nne za kupima joto. Amesema wamekabidhi box 20 za sabuni za maji ya kunawia mikono, middle’s Paddle hand wash-facilities 35 Matanki ya kuhifadhia maji kwenye vifaa vya kunawia mikono 20, Chlorine powder kilo 126, Chlorine tablets kilo 5 za Kuna vitakasa mikono mabox 24, PPE 63, gloves boxes 83, spika 3 kwa ajili ya matangazo ya kuelimisha juu ya corona, vipeperushi 144, vienye ujumbe wa kuelimisha juu ya corona pamoja na bronchure 200 na bango 1na Face shield 333.
Amesema mbali na vifaa hivyo wamejikita katika kutoa elimu kwa njia ya bodaboda ambazo watatumia vipaza sauti kucheza sauti iliyorekodiwa na wataalamu wa afya juu ya namna ya kujikinga na virusi vya corona. Ndg. sakafu amesema watutumia wataalamu wa Halmashauri kutoa elimu ya corona kwa wananchi na watapita kwenye vijiji na magari, kutembelea kaya kuelimisha watu juu ya namna ya kujikinga na corona.
Mh. Theresia Mahongo Mkuu wa wilaya ya Karatu (kushoto) na Katibu tawala wa wilaya ya Karatu Ndg. Abbas Kayanda wakikagua vifaa vilivyoletwa na CSEE
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa