Na Tegemeo Kastus
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo amesema swala la kulipa madiwani posho lazima lisimamiwe na malipo yalipwe kulingana na uhalisia wa mahali diwani anapotoka. Mtu anayetoka umbali wa km 80 hawezi kulipwa sawa na mtu anayetoka km 5 au 10. Amesema uongozi unataka haki ukicheza na principal uongozi utayumba.
Hayo yamesemwa katika kikao maalumu cha madiwani kujadili ripoti ya mkaguzi mkuu wa serikali.Kutokana na changamoto hiyo mkuu wa mkoa Mhe. Gambo ameunda tume kuchunguza na kutoa mapendekezo dhidi ya sakata hilo la posho za madiwani.Tume hiyo imehusisha watu mbalimbali na itafanya kazi ndani ya juma moja ili kubaini namna sahihi ya kulipa madiwani kulingana na maeneo wanapotoka.
Mhe. Gambo amesema tume hiyo baada ya kufanya uchunguzi wa nyaraka na kubaini uhalisia na baadae kuwasilisha kwa Mkuu wa wilaya ya karatu. Mkuu wa wilaya atamuita Mkurugenzi pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri na viongozi wa chama. Mh. Gambo amesema ajenda anazozisimamia ni pamoja na kila mtu kulipwa kutokana na umbali anapotoka. Amesema utaratibu wa kuwafuata madiwani katika maeneo wanayotoka haupo amesema madiwani watumie usafiri wa umma na watoe vielelezo ili waweze kupata stahiki zao kulingana na mazingira wanayotoka.
Mwenyekiti wa Halmashauri Mh.Emmanuel Gege amesema ni aibu kwa baraza kujadili maslahi binafsi. Amesema ni vyema kiongozi aliyetokana na wananchi ajadili mambo ya maendeleo, amesema hizi tamaa binafsi ndizo zinatufikisha hapa tulipo amesema kama Mwenyekiti hiyo si sehemu ya vikao anavyosimamia. Amesema madai ya maslahi binafsi niyakikundi cha watu kisichopungua watatu au wane
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya karatu Ndg. Waziri Mourice amesema wakati anaapokea majukumu ya ukurugenzi wa Halmashauri amekuta Waheshimiwa madiwani wa Mjini na Vijijini wote wanalipwa night mbilimbili. Amesema alipoanza kulibadili swala hilo madiwani wakaanza kususia vikao vya Halmashauri. mvutano huo ulisababisha Mkurugenzi kupewa siku za kuondoka. Ameongeza kusema waraka wa serikali haujadiliwi lakini madiwani hawa walikuwa wanajadili waraka wa serikali.
Ofisi ya Takukuru wilaya ya Karatu ilichunguza ikabaini kuna madiwani kweli walilipwa kinyume na utaratibu. Ofisi ya Takukuru wilaya ilihoji diwani mmoja baada ya mwingine amesema baadhi ya madiwani wamerejesha zile fedha. Amesema baada ya waheshimiwa kuitwa na Takukuru wakakana kwamba hajawahi kuona waraka unaotoa maelekezo ya malipo. Amesema jambo hilo limesababisha Mkurugenzi pamoja na Afisa utumishi kuanza kuzirejesha hizo fedha zilizoliwa na madiwani.
Waheshimiwa Madiwani katika kikao maalumu cha baraza kujadili taarifa ya Mkaguzi mkuu wa serikali
Akiwa anachangia mjadala huo Mh. Ally Lorry amesema hoja za mdhibiti mkuu wa serikali haziwezi kuisha kutokana na ushahidi wa mazingira. Amesema kuna waraka wa serikali kuhusu namna ya kulipa posho za madiwani lakini hautafsiriwi vizuri. Amesema lazima mazingira ya mashaka yasiwepo ya namna posho zinavyolipwa ili kuondoa hoja kwa mwaka ujao wa fedha.
Naye Mh. Sophia Margwe amesema wameona waraka wa serikali mwezi wa tisa 2019, lakini Posho za madiwani zimekuwa zinalipwa tofauti tofauti. Amesema kuna madiwani wanalipwa laki na sabini; wengine elfu tisini na tano, wengine elfu sabini huko Mang’ola mimi Endamaghan nalipwa laki moja lakini diwani wa Mbulumbulu analipwa laki na arobaini na tano. Mh. Sophia amesema hana night hata moja, amesema swala la posho linagawa madiwani wa Karatu.
Akichangia hoja hiyo Mh. John Lucian amesema tumekuja kama wawakilishi wa wananchi lakini sasa tunadai posho. Amesema Ofisi ya mkuu wa Mkoa ipo wazi ofisi ya Mkuu wa wilaya ipo wazi ni vyema tukatumia kikao kujadili mambo yaliyodhamiriwa kwenye kikao. Amesema tumemubebesha Afisa utumishi mzigo ambao sio wake, na tumebakiza wiki moja na tunaondoka na mzigo wa laana za watumishi. Agenda hii ilikuwepo vikao vya baraza la madiwani lilopita na walishawahi kugomea vikao kutokana na madai ya posho, amesema tulishawahi kukaa kama kamati juu ya hoja ya posho na likajadiliwa zaidi ya masaa mawili.
watendaji wakiwa katika kikao maalumu cha baraza kujadili taarifa ya Mkaguzi mkuu wa serikali
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa