NA TEGEMEO KASTUS
Watumishi mnapaswa kujiepusha na vitendo vya ubadhilifu utoro na utovu wa nidhamu katika utendaji kazi.Ili utendaji kazi uwe na ufanisi tunapaswa kufuata maadili ya utumishi kuepuka migogoro mahali pakazi. Viongozi wa vyama vya wafanyakazi na watumishi ni vyema kuhimizana kujua na kuzingatia sheria za utumishi. Wajibu wa serikali ni kulinda haki za mfanyakazi na katika kutatua migogoro viongozi wa vyama vya wafanyakazi na waajiri mjenge tabia ya kukaa kwa pamoja kutatua matatizo.
Hayo yemesemwa na Katibu tawala wa wilaya ya Karatu Bi. Faraja Msigwa aliyemuwakilisha mgeni rasmi katika sherehe za siku ya wafanyakazi Mkuu wa wilaya ya Karatu. Kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya wafanyakazi ni “maaslahi bora mishahara juu, kazi iendelee.”Amesema swala la mahusiano kati ya muajiri na watumishi ni muhimu sana, ndio maana tunahimiza vyama vya wafanyakazi kukutana mara kwa mara na watumishi ili kuondoa changamoto za kinidhamu mahali pakazi. Akizungumzia swala la watumishi wa volt 5000 kushindwa kupelekewa makato yao kwenye mfuko wa Pspf, Bi, Msigwa amemulekeza Mkurugenzi mtendaji kuanza kulishughulikia swala hilo mapema. Amesema limekuwa swala la muda mrefu na linasababisha watumishi hao kukosa fao la uzazi na matibabu.
Watumishi wakipewa zawadi mbalimbali wakati wa sherehe ya siku ya wafanyakazi
Bi, Msigwa amesema waajiri wanapaswa kuwapa watumishi stahiki zao kwa wakati ili wafanyakazi waweze kufanya kazi kwa moyo. Amesema kuna taarifa za watumishi kukosa vifaa hasa kwa wafanyakazi wa mashambani na mahotelini kwenye sekta binafsi. Viongozi wa vyama vya wafanyakazi simamieni na muhakikishe watumishi wa sekta binafsi wanafanya kazi katika mazingira salama. Amesema kama viongozi watashauri waajiri na wakapuuzia kwa kuonesha kutokujali usalama wa watumishi katika maeneo ya kazi ni vyema kuwasilisha malalamiko kwa watu wa OSHA. Watu wa OSHA wapo kwa ajili ya kulinda na kusimamia usalama wa watumishi katika maeneo ya kazi.
Bi, Msigwa amesema anajua watumishi wengi kwa ujumla ni watendaji kazi wazuri, lakini kwa sababu ya vigezo vilivyowekwa tunapata mtu mmoja kama mshindi. Amesema kumpatia mfanyakazi zawadi ya utendaji bora ni jambo jema, ni vyema likaenziwa na likaboreshwa zaidi. Amesema ni jambo jema linaloongeza ari ya kufanya kazi na wale ambao hajapata zawadi wasivunjike moyo, wote ni wafanyakazi bora.
Mwl Laizer kutoka Marang akipokea zawadi
Akizungumza katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Ndg. Waziri mourice amesema serikali kwa mwaka huu wa fedha Halmashauri imepata barua ya kupandishwa vyeo. Amesema vyeo hivyo vitapandishwa kuanzia mwaka 2017-2018 mwaka 2018-2019 mwaka 2019-2020 na mwaka 2020-2021.
Katibu wa chama cha walimu Relief Julius katika risala yake kwa mgeni rasmi amesema kumekuwa na utofauti mkubwa wa mishahara kati ya watumishi wa kawaida na watumishi wa wateule wa rais na wakuu wa sekta, amesema tofauti hiyo imekuwa ikipunguza ari ya utendaji kazi wa watumishi. Utofauti huo wa mshahara upungue kwa kuongeza kima cha chini cha mshahara, Mwl Julius amesema maslahi ya wanasiasa kutofautina kwa kiasi kikubwa na Maslahi ya wataalamu kumesabisha wataalamu wengi kujiingiza kwenye siasa hivyo kupunguza nguvu kazi ya wataalamu.
wafanyakazi katika picha tofauti wakipokea zawadi baada ya kuibuka vinara kwa utendaji mzuri wa kazi
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa