NA TEGEMEO KASTUS
Wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wakiongozwa na mkuu wa wilaya ya Karatu wamefanya ziara katika eneo la mnadani Karatu. Wametembelea na kuona eneo la machinjio ya mnadani na eneo lilojengwa choo cha umma kinachosimamiwa na Halmashauri.
Mh. Abbas Kayanda Mkuu wa wilaya ya Karatu ametoa maelekezo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Karatu kuhakikisha milango na madirisha ambayo imeharibiwa na kuibiwa katika maliwato hayo yanarudishwa na kuwekwa ifikapo tarehe 24 mwezi wa nane mwaka huu. Mh. Kayanda ameelekeza miundo mbinu ya maji ambayo nayo ilikuwa imeondolewa ikarabatiwe na kuwekwa katika Maliwato hayo.
Hali ya vioo vya madirisha ilivyo katika maliwato hayo baada ya kuvunjwa na milango kung'olewa
Mh. Kayanda amesema lazima mali zote za umma zitunze na kulindwa, amekemea uzembe uliofanywa katika jengo hilo la maliwato baada kwa kukosa Mlinzi anayelinda Maliwato ya eneo hilo, jambo lilotoa mwanya kwa watu wasio waaminifu kuvunja madirisha na kuiba milango ya maliwato yaliyojengwa katika eneo hilo la mnada. Mh. Kayanda ametoa maelekezo kwa Mkurugenzi Mtendaji kurekebishwa miundo mbinu ya Machinjio ya mnadani na kuliweka eneo hilo katika mazingira ya usafi pamoja na kulinda miundo mbinu ya machinjio.
Mh. Kayanda ametoa maelekezo kwa Afisa mazingira kuhakikisha mji wa Karatu unakuwa msafi, amesema bado katika swala la usafi Karatu tupo nyuma. Watu wanatupa taka hovyo amesema lazima usafi usimamiwe ili siku moja tuwe mfano wa Halmashauri zenye mazingira safi hasa ukizingatia mji wa Karatu ni mji wa kitalii.
Mh. Kayanda ametembelea eneo la soko kuu la mjini wa Karatu ambalo ujenzi wa vizimba 202 unaendelea kwa awamu. Pamoja na eneo la mbele ambalo limeachwa kwa ajili ya ujenzi wa maduka. Mh. Kayanda ametoa maelekezo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri kuhakikisha ujenzi huo unakamilika haraka na kwa wakati ili wakati vizimba vya kwanza vianamaliziwa kuwekwa plasta vizimba vilivyobakia vianze kujengwa ili wananchi waanze kulitumia soko mapema iwezekanavyo. Mh. Kayanda ametoa ameelekeza miundo mbinu ya umeme iwe tayari kabla wafanyabiashara hawajaanza kuingia na kulitumia soko.
Mkuu wa wilaya Mh. Abbas Kayanda akikagua maendeleo ya ujenzi wa Vizimba katika eneo la soko kuu Karatu.
Mh. Kayanda ametembelea jengo la Halmashauri la zamani ambalo awali lilikuwa halijafanyiwa ukarabati kwa muda mrefu. Mh. Kayanda ameona jengo hilo likiwa limefanyiwa ukarabati wa ofisi pamoja na samani za ofisi zikiwa katika hali nzuri na limekuwa tayari kutumiwa kama ofis ya Afisa mamlaka ya mji mdogo wa Karatu. Mh .kayanda amepongeza Mkurugenzi Mtendaji kwa ukarabati Mzuri amemuelekeza Afisa Mji mdogo wa Karatu pamoja na wafanyakazi wa mamlaka ya mji mdogo kulitumia na kuendelea kutunza miundo mbinu ya jengo pamoja na samani zilizopo katika jengo hilo.
Mkuu wa wilaya ya Karatu. Mh. Abbas Kayanda akikagua Ukarabati wa Ofis ya Mamaka ya Mji mdogo Karatu.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa